Zanzibar
Idara ya Uhamiaji Zanzibar, mapema wiki hii imeungana na taasisi nyingine za serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na taasisi binafsi katika maonesho ya biashara ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kuadhimisha miaka (57) ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar.
Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika ufunguzi wa maonesho hayo, Mhe. Samia ameipongeza serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kudhamiria kukuza uchumi wa buluu kwa kutumia rasilimali za bahari.
Pia Mhe. ameitaka serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuyadumisha maonesho hayo ya biashara na kuongeza idadi ya washiriki.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kukagua mabanda ya maonesho |
Wananchi wa Zanzibar wakipata Huduma za Ki-Uhamiaji katika tamasha la saba la bishara zanzibar |
(Picha zote na kitengo cha uhusiano afisi kuu Zanzibar) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni