Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Oktoba 2019

Zimebaki siku 90

EPUKA MSONGAMANO: ZIMEBAKI SIKU 90 KUFIKA MWISHO WA MATUMIZI YA PASIPOTI ZA ZAMANI (MRP). BADILI SASA KUPATA PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI. #ePassport, #eVisa, #ePermit, #eBorderManagementSystem

30 Oktoba 2019

Dkt. Makakala aridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la Uhamiaji Dodoma.








Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara hiyo, amefanya ukaguzi wa kazi ya ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, jijini Dodoma. Katika ukaguzi huu Dkt. Makakala ambaye aliambata na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogero, amesifu kazi nzuri inayofanywa na wahandisi wa Kampuni ya Kizalendo ya SUMA JKT ambayo ndiyo iliyopewa zabuni ya ujenzi wa jengo hilo la ghorofa nane ambalo linalotarajiwa kuwa la kuvutia jijini humo.

Kazi ya ujenzi wa sehemu ya ardhini ya jengo hilo imekamilika na kwa sasa maandalizi ya kumwaga zege la jamvi la ghorofa ya chini yamekamilika na tayari Mshauri Mwelekezi wa Mradi huo ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi ametoa idhini ya kumwaga zege ili kuruhusu hatua zaidi za ujenzi kuendelea.


Ujenzi wa Jengo hilo uinatarajiwa kukamilika ndani ya muda wa miezi 18, na kwa mujbu wa Meneja Mradi, Kanali Zablon Mahenge amesema ujenzi unakwenda kwa kasi na umakini mkubwa na kwamba kazi itakamilika kwa wakati na ubora wa hali ya juu.


25 Oktoba 2019

Dkt. MAKAKALA AMPONGEZA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2019









Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amempongeza Mkaguzi  Msaidizi wa Uhamiaji Mzee Mkongea Ali  kwa kuiwakilisha vyema Idara ya Uhamiaji katika Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2019.

“Nakupongeza sana kwa kazi nzuri uliofanya katika Taifa letu. Nimefurahi sana kwa uwakilishi wako uliotukuka, kwa kweli umeibeba vyema bendera ya Uhamiaji, unastahili pongezi za dhati, pamoja na kwamba uko likizo lakini nimeona nikuite uje nikupongeze” Alisema Dkt. Makalala

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi Mzee Mkongea alimshukuru Kamishna Jenerali, Makamishna na Viongozi waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kwa Miongozo, Ushauri na Maelekezo yao ya mara kwa mara yaliyomuwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wote wa mbio hizo.

Mzee Mkongea Ali ambaye ni Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mjini Magharibi alikuwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019 ambapo ameifanya kazi hiyo kwa bidii, uadilifu, utiifu na uzalendo hadi kufikia kilele cha mbio hizo na kuzimwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mjini Lindi tarehe 14 Oktoba 2019.

18 Oktoba 2019

UHAMIAJI YASHIRIKI MAONYESHO YA UTALII YA “SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO






























Katibu mkuu kiongozi  Balozi John kijazi leo amezindua maonyesho ya Utalii ya” SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO katika viwanja vya mlimani city Dar es salaam.

Maonyesho hayo ambayo yameanza leo tarehe18 yatamalizika tarehe 20 mwezi huu yamehusisha taasisi mbalimali ikiwemo idara ya uhamiaji ambapo kama kawaida imeendelea kutoa huduma kwa wageni waalikwa pamoja na wananchi wanaohudhulia maonyesho hayo.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo Balozi Kijazi amesifu maandalizi ya maonyesho hayo na kuwataka wanachi kujitokeza kujua na kujifunza mambo mbalimbali kupitia maonyesho hayo ambayo yanatarajiwa kumalizika Jumapili.

Pia balozi kijazi ameongeza  Maonyesho hayo yamesaidia sana kukuza sekta ya utalii  ikiwa ni pamoja na kuongeza  pato la taifa kupitia  sekta ya utalii nchini.

12 Oktoba 2019

Imarisheni doria maeneo yenu” Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala ametoa agizo hilo alipotembelea ofisi ya Uhamiaji Mkoa Katavi ambapo pamoja na kupata taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo na kusikiliza changamoto mbalimbali, aliendelea kusisitiza watumishi wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

“Nawataka muimarishe doria katika maeneo yenu hasa katika kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi wa serikali za mitaa, maeneo haya yana makambi ya wakimbizi na walowezi. Hakikisheni hawajiingizi kwenye uchaguzi aidha kugombea nafasi za uongozi au kupiga kura.” Aliagiza Dkt. Makakala akiwa Namanyere.

“Mnafanya kazi nzuri sana pamoja na changamoto zilizopo, kila ofisi au kituo nInachopita maneno yangu ni yale yale nakumbusha tu kuwa kila mmoja ajitambue kuwa anatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na kuzingatia motto yetu ya Nidhamu, Upendo na Mshikamano miongoni mwenu, Uwajibikaji katika utendaji kazi wenu na kukataa rushwa” alisisitiza Dkt. Makakala.


Afisa Uhamiaji Mkoa Katavi, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Vicent Haule akisoma taarifa ya Utendaji kazi mkoa Katavi mbele ya Kamishna Jenerali Dkt. Makakala.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya uhamiaji mkoa Katavi alipotembelea mwanzoni mwa wiki hii.



Maafisa Uhamiaji mkoa wa Katavi wakimsikiliza Kamishna Jenerali 





Kamishna Jenerali Dkt. Makakala akimsikiliza Afisa Uhamiaji Wilaya ya Nkasi Mrakibu Joseph Bulali wakati alipotembelea ofisi hiyo kuongea na watumishi
Add caption
Kamishna Jenrali akisalimiana na Maafisa wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa alipotembelea ofisi hiyo.