Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna
Makakala na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara hiyo, amefanya
ukaguzi wa kazi ya ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji
eneo la NCC, jijini Dodoma. Katika ukaguzi huu Dkt. Makakala ambaye
aliambata na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogero, amesifu
kazi nzuri inayofanywa na wahandisi wa Kampuni ya Kizalendo
ya SUMA JKT ambayo ndiyo iliyopewa zabuni ya ujenzi
wa jengo hilo la ghorofa nane ambalo linalotarajiwa kuwa la
kuvutia jijini humo.
Kazi ya ujenzi wa sehemu ya ardhini ya jengo hilo
imekamilika na kwa sasa maandalizi ya kumwaga zege la jamvi la ghorofa
ya chini yamekamilika na tayari Mshauri Mwelekezi wa Mradi huo ambaye
ni Chuo Kikuu cha Ardhi ametoa idhini ya kumwaga zege
ili kuruhusu hatua zaidi za ujenzi kuendelea.
Ujenzi wa Jengo hilo uinatarajiwa
kukamilika ndani ya muda wa miezi 18, na kwa mujbu wa Meneja
Mradi, Kanali Zablon Mahenge amesema ujenzi unakwenda kwa kasi
na umakini mkubwa na kwamba kazi itakamilika kwa wakati
na ubora wa hali ya juu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni