Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dkt. Anna Peter Makakala ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa
Idara ya Uhamiaji katika Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza na Watumishi hao,
Kamishna Jenerali amewasihi kujiepusha na vitendo vya rushwa na kufanya kazi
kwa weledi na bidiii ili kwenda sambamba na kasi ya serikali ya Awamu ya Tano
katika kuwaletea wananchi wake maendeleo na kukuza uchumi wa nchi yetu.
“Idara
ya Uhamiaji ina jukumu kubwa la kukuza sekta za Utalii na Uwekezaji katika nchi
yetu hivyo tunatakiwa kuwahudumia wageni wanaoingia na kuishi nchini bila
vikwazo vinavyoweza kurudisha nyuma ustawi wa sekta hizo” amesitiza
Dkt. Makakala.
Kwa upande wake Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Shaaban Omari ameeleza kuwa Idara
inaendelea na mapambano dhidi ya Wahamiaji kwa kuwashirikisha Viongozi wa Serikali
za Mitaa na Kata.
Viongozi hao Kata na Vijiji wanapatiwa
Elimu ya Uhamiaji ili kuwajengea uelewa katika masuala ya Kiuhamiaji ikiwa ni
maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kutekeleza Mpango Mkakati wa Mapambano
dhidi ya Wahamiaji haramu (Pekenyua Fukunyua) unaondelea nchi nzima kwa sasa.
Akiwa katika ziara hiyo Mkoani
Mbeya, Dkt. Makakala ametembelea na kukagua Ofisi za Uhamiaji katika Vituo vya Uwanja
wa Ndege wa Songwe pamoja na Mpaka wa Kasumulu.
Kesho Jumamosi Oktoba 5,
2019, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji atahudhuria Uzinduzi wa Kituo cha pamoja
cha utoaji huduma za mpakani (OSBP) katika Mpaka wa Tunduma Mkoani Songwe
ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli.
Kaimu Mfawidhi wa kituo cha Uhamiaji Kasumulo akimuonesha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji eneo litakalojengwa kityoo cha Mpaka wa Pamoja (OSBP). |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiongea na raia wa DRC Bwana Jeane Pierre aliyekuwa akipata huduma za Uhamiaji katika mpaka wa Tunduma |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha Uhamiaji Tunduma mkoani Songwe |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni