Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

01 Septemba 2022

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Aweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Chuo Kipya cha Uhamiaji na kufunga Mafunzo ya awali ya Askari Wapya wa Uhamiaji.

Na. Konstebo Amani Mbwaga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 15 Agosti 2022 ameweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba kilichopo Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga na kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Uhamiaji Kozi Na. 01/2021/2022.

Mhe. Rais amelipongeza Jeshi la Uhamiaji nchini kwa kuanzisha chuo chake cha mafunzo na kumtaka Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kuwarudisha Mafunzoni Maafisa na Askari waliopo kazini ili chuo kiendeleee kutumika ipasavyo lakini pia na kuwajengea uwezo katika kundelea kutekeleza majukumu kwa Ufanisi na Weledi wa hali ya juu.

Pia Mhe. Rais ametaka kuwepo kwa Mafunzo ya pamoja baina ya Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini ili kupata uzoefu wa Pamoja.

Kwa Upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amemshukuru Mhe. Rais kwa kwa kuwa Mgeni Rasmi na Kuhitimisha Mafunzo ya awali ya Askari wa Uhamiaji Snjari na kuweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa chuo cha Mafunzo ya Uhamiaji.

Dkt. Makakala aliwapongeza na kuwashukuru pia Maafisa, Askari na watumishi Raia kwa kujitolea kuanza kuchangia ujenzi wa chuo hicho sambamba na wadau mbalimbali ambapo wengine walichangia vifaaa.

Aidha Dkt. Makakala amesema maelekezo yote ya Mhe. Rais yamepokelewa kwa mikono miwili na tayari kwa utekelezaji.

 

Haya ni Mafunzo ya kwanza kwa Jeshi la Uhamiaji tangu kuanza kujitegemea ambapo askari wa Uhamiaji 818 kati ya 820 wamehitimu Mafunzo hayo na kupewa jina la Operesheni Ujenzi.

Mafanikio haya ya ujenzi wa chuo kipya cha mafunzo ya Uhamiaji yametokana na Uongozi imara chini ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala  na wasaidizi wake wakiwemo Maafisa na Askari wa Jeshi la Uhamiaji ambao kwa mara ya kwanza walichangia fedha zaidi ya milioni themanini na kuanza ujezi huo ambao kwa sasa chuo kina uwezo wa kuendesha kozi yenye Maafisa na  Askari  zaidi ya 1000 kwa wakati mmoja.

 

#UhamiajiUsalamanaMaendeleo

MATUKIO KATIKA PICHA