Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

25 Oktoba 2020

Wana HamaHama Bendi yatia fora Tamasha la Amani la Majeshi ya Ulinzi na Usalama

25 Oktoba 2020

Dodoma, Tanzania

Bendi ya Uhamiaji maarufu kama Wana HamaHama Bendi imeshiriki Tamasha la Amani la Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Nyerere jijini Dodoma na kutoa burudani safi kwa wapenzi wa muziki jijini hapa waliofika katika Tamasha hilo  lililoandaliwa na Chama cha muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA)

 

Bendi hiyo ya Uhamiani inayomamiwa na meneja ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Denis Kimaro imeimba nyimbo zinazohamasisha Uzalendo na Amani hasa wakati huu ambapo Taifa linaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

 

“Bendi yetu imefanya vizuri sana leo maana tumetambulisha nyimbo mpya mbili zinazo hamasisha uzalendo na amani kati ya nyimbo nne tulizoimba, wenzetu wa vyombo vingine vya ulinzi  wameona jinsi gani tulijiandaa kutoa burudani ikizingatiwa kuwa mara yetu ya kwanza kuimba kwenye jukwaa moja na bendi nyingine. Namshukuru Afande CGI kuifufua bendi hii ambayo ilifufa tangu miaka ya 1990, na pia kwa kutuwezesha kuwa na vifaa vya kisasa vya muziki. Aidha tunamshukuru msimamizi mkuu Mrakibu Paul Mselle kwa ushauri na malezi mazuri.Tunaahidi mengi mazuri kutoka kwa Wana Hamahama” alieleza Afisa Uhamiaji huyo mara baada ya Tamasha.

 

Ikumbukwe kwamba, Idara ya Uhamiaji iliwahi kuwa na Bendi iliyotamba miaka ya mwishoni ya 70 hadi mwanzoni mwa 90 baadaye bendi ilikufa na kufufuliwa mwaka 2019 na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dtk. Anna Makakala


 

23 Oktoba 2020

CGI Dkt. ANNA MAKAKALA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala siku ya Alhamisi tarehe 22 Oktoba 2020, amefanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma. 

Uhamiaji Dkt. Makakala atembelea na kukagua maendeleo ya

Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma. Katika ziara hiyo,
Kamishna Jenerali ailiipongeza Kampuni ya Suma JKT kwa kasi na kazi nzuri ya
ujenzi wa jengo hilo.12 Oktoba 2020

Chuo cha Uhamiaji chaendelea kutoa Mafunzo ya Masuala ya Kiuhamiaji kwa Taasisi na Sekta Binafsi

Moshi, Kilimanjaro
Idara ya Uhamiaji kupitia chuo chake Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kimeendelea kutoa mafunzo kwa Taasisi za Umma na Sekta binafsi ili kuwajengea uwezo juu ya masuala ya Uhamiaji 

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo siku ya Ijumaa, Kaimu Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo amesema  lengo la kuwapa mafunzo ni kuwajengea uwezo wa kuzifahamu Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia masuala ya Uhamiaji hapa nchini.

Aidha mafunzo hayo kwa ujumla yalilenga pia katika kuwajengea uelewa na maarifa washiriki  ili kuwawezesha kuwa na weledi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi. 

"Wengi wenu ni Maafisa Utumishi katika Taasisi au Makampuni ambapo mnaajiri wageni, hivyo ni wajibu wetu kuwaelimisha taratibu mbalimbali ili wageni wenu waishi na kufanya kazi nchini pasipo kuvunja sheria za Uhamiaji." Alisema Towo.

Hata hivyo DCI Towo aliendelea kueleza kwamba katika masomo yao washiriki walikuwa wakijadidili hoja mbalimbali  na baadhi tayari zimechukuliwa na zinaingia katika Taarifa ya  kuwasilisha kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala kwa ajili ya maamuzi ambapo utekelezaji wake utafuata na utaleta manufaa mengi kwenye Idara na Nchi kwa Ujumla.

Nae mmoja wa wahitimu kutoka Kampuni ya Fluiconecto Tanzania Ltd ya mjini Mwanza Bi. Azza Hilal alisema mafunzo haya yamemuwezesha kujua taratibu zinazotakiwa kufuata ili kumuajiri raia wa kigeni katika kampuni yake.

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza Oktoba 5 na kumalizika Ijumaa Oktoba 9 huku yakishirikisha Washiriki 30 ambao wamehitimu na kupatiwa vyeti vya ushiriki.

Washiriki hao Walipata pia fursa ya Kutembelea Hifadhi ya  Mlima Kilmanjaro (KINAPA) na baadae kutoa zawadi ya Keki kwa Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo

Kwa Ujumla Mafunzo haya ni mwendelezo wa Programu za  Idara ya Uhamiaji kupitia chuo chake cha TRITA katika kuwaelimisha wadau wanaohusika na raia wa kigeni hapa nchini sanjari na kutoa huduma za Ki-Uhamiaji zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa na hatimae kulinda Usalama wa Taifa ili Kukuza Maendeleo ya Kiuchumi kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Kaimu Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo Akitoa Cheti kwa mmoja wa Washiriki wa Mafunzo


Washiriki wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Kaimu Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo (Hayupo Pichani)

Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Chuo cha Uhamiaji TRITA-Moshi Mrakibu Msaidizi (ASI)Leslie Mbotta Akiwashukuru Washiriki kwa kuonesha ushirikiano wa kutosha wakati wa Mafunzo yaoWashiriki wa Mafunzo ya Ki-Uhamiaji TRITA wakiwa katika Picha ya Pamoja (katikati) ni Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

08 Oktoba 2020

CGI Dkt. Anna Makakala Ahudhuria Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam.

Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala Mapema leo hii  amehudhuria Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es salaam 

Hafla hiyo iliongozwa na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera na Mwenyeji wake Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Aidha tukio hilo limehudhuriwa pia na Wakuu wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama sanjari na Mawaziri mbalimbali Makatibu wakuu wa wizara na Viongozi wengine waandamizi wa serikali bila kuwasahau wananchi wa Jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa Ujumla

Kituo hicho cha Mabasi Kitagharimu Zaidi ya Bilioni 70 za Kitanzania ambazo ni fedha za ndani, huku lengo kuu likiwa ni kuwahudumia Wananchi wa Tanzania na Wageni wengine kutoka Nchi Mbalimbali za Jirani na zile za SADC.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Muonekano wa Ujenzi wa Kituo Kipya cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es salaam Ukiendelea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Akiongea na Wananchi wa Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam

Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera akiongea na Wananchi wa Dar es salaam wakati wa Uuwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akipokea maelezo ya namna Kituo cha Mabasi Kitakavyokuwa  baada ya kuhudhuria Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es salaam 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jaffo akitoa Maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo Kipya cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis


Muonekano wa Jengo la Kituo cha Mabasi Mbezi Luis Ujenzi Ukiendelea


Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara Waliohudhuria Hafla hiyo


Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliohudhuria Hafla hiyo

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akimuaga Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera (Hayupo Pichani) baada ya kumaliza tukio la  Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akimuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumaliza tukio la  Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam.Kamishna wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Suleiman Mzee akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya  Ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaa

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  Dkt. John Kijazi  (Kulia) akiteta Jambo na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol)  Balozi Kanali Wilbert Ibunge baada ya Kuhitimisha Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi katika  Kituo Kipya cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam 


(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)