Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Aprili 2018

UHAMIAJI ILIVYOSHIRIKI SHEREHE ZA MUUNGANO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala aliiongoza Idara ya Uhamiaji kwenye Sherehe za Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma siku ya Alhamisi tarehe 26 Aprili 2018.

Katika sherehe hizo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji alikuwa ni miongoni mwa wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama waliohudhuria.

Sherehe hizo zilipambwa kwa gwaride kutoka vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na Usalama, vijana wa halaiki pamoja na vikundi vya sanaa na ngoma za asili.

Kauli mbiu ya Miaka 54 ya Muungano ni “Muungano wetu ni Mfano Duniani, Tuuenzi, Tuulinde, Tuimarishe na Kuudumisha Kwa Maendeleo ya Taifa Letu”

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akisalimiana na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Sherehe za kuadhimisha Miaka 54 ya Muungano Tanganyika na Zanzibar
 

 

Uzinduzi Wa E-Passport Mkoa Wa Dodoma

Kamishna Jenerali Wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala Anawaalika Watanzania Wote Na Wakazi Wa Jiji La Dodoma Kwenye Uzinduzi Wa Huduma Za  E-Passport Katika Jiji Hilo SIKU YA JUMATATU TAREHE 30/04/2018, Kuanzia Saa Tatu Asubuhi Kwenye Ofisi Za Uhamiaji Dodoma.


25 Aprili 2018

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji atoa salamu za Miaka 54 ya Muungano


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala pamoja na Maafisa na Askari Wote wa Idara ya Uhamiaji kwa pamoja wanaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na Watanzania Wote katika kuadhimisha Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar


10 Aprili 2018

Namna Idara ya Uhamiaji inavyopambana na suala zima la Uhamiaji Haramu


Kaimu Kamishna wa Uhamiaji (Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka) Hosea Kagimbo akiongea katika kipindi cha Semakweli katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten namna Idara ya Uhamiaji inavyotekeleza majukumu yake ya udhibiti na usimamizi wa mipaka kwa lengo la kudhibiti Wahamiaji Haramu nchini.