Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Aprili 2018

UHAMIAJI ILIVYOSHIRIKI SHEREHE ZA MUUNGANO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala aliiongoza Idara ya Uhamiaji kwenye Sherehe za Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma siku ya Alhamisi tarehe 26 Aprili 2018.

Katika sherehe hizo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji alikuwa ni miongoni mwa wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama waliohudhuria.

Sherehe hizo zilipambwa kwa gwaride kutoka vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na Usalama, vijana wa halaiki pamoja na vikundi vya sanaa na ngoma za asili.

Kauli mbiu ya Miaka 54 ya Muungano ni “Muungano wetu ni Mfano Duniani, Tuuenzi, Tuulinde, Tuimarishe na Kuudumisha Kwa Maendeleo ya Taifa Letu”

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akisalimiana na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Sherehe za kuadhimisha Miaka 54 ya Muungano Tanganyika na Zanzibar
 

 

Maoni 1 :