Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali
Jacob Kingu amefunga mafunzo ya upandishwaji vyeo kwa askari na maafisa
uhamiaji yaliyofikia tamati siku ya tarehe 27 Julai 2018. Mafunzo hayo ya miezi
mitatu yaliyofanyika Shule ya Polisi Moshi yalishirikisha askari na maafisa
uhamiaji 507 yalikuwa ni moja ya hatua ya kupanda cheo.
Awali, Meja Jenerali Kingu alikagua vikosi na baadae Gwaride
maalumu la kufunga mafunzo kutoka kwa wahitimu lilipita mbele ya mgeni rasmi
kutoa heshima za ambapo wananchi waliofika kushuhudia sherehe hizo
walishangilia kwa nguvu na vigelegele wakifurahia gwaride hilo.
|
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Mkuu wa Shule ya Polisi pamoja na wakufunzi wa shule hiyo. |
|
Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Mrakibu Mwandamizi Bazo akisalimiana na Katibu Mkuu Meja Jenerali Kingu |
|
Mgeni rasmi Meja Jenerali Kingu na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala (kushoto) wakitoa heshima zao kwa gwaride. |
|
Gadi ya Askari na Maafisa Uhamiaji likipita mbele ya mgeni Rasmi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Upandishaji vyeo katika shule ya Polisi. |
|
GAadi ya Askari na Maafisa wa kike ikiongozwa na Mkufunzi Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Salma Panja likipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zake. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni