Baadhi ya Maafisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Makao Makuu
wameanza mafunzo ya siku tatu juu ya Usimamizi wa Vihatarishi (Risk
Management) katika jengo la Makao Maku ya Idara hiyo Kurasini jijini Dar es
salaam.
Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji
Andrew Malyeta ambaye pia ni Mratibu wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Idara hiyo
amesema lengo kuu la mafunzo haya ni kuwapa uelewa watumishi katika Usimamizi wa Vihatarishi kutokana na Muongozo wa Usimamizi wa Vihatarishi
katika Sekta ya Umma (Guidelines for
Developing and Implementing Institutiona Risk Management Framework in Public
Sector, December 2013) pamoja na Sera
ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Idara ya Uhamiaji (Institutional Risk Management Framework and Guide for the Immigration
Department, 2016).
“Kwa muongozo na sera hio tunategemea maafisa
wetu watajifunza mambo muhimu sana katika utendaji kazi wao wa kila siku ambayo
ni Muundo wa Usimamizi wa Vihatarishi, Wadau wa Usimamizi wa Vihatarishi,
Majukumu ya mabingwa wa Vihatarishi, Hatua za Usimamizi wa Vihatarishi,
Mgawanyo wa Vihatarishi, rejesta za Viharatishi pamoja na Nyenzo zinazotumika
katika Usimamizi wa Vihatarishi’’ aliongeza Mrakibu Msaidizi
Malyeta.
Mafunzo haya yanafanyika kwa ushirikiano na wawezeshaji
katika Usimamizi wa Vihatarishi kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana
Josephat Kajonga ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi
na Bi. Lulu Ishengoma ambaye ni Afisa kutoka Kitengo cha Usimamizi wa
Vihatarishi.
Jumla ya Watumishi (askari na kada ya kawaida) 20
wanahudhuria mafunzo haya kutoka vitengo vya Uhasibu, BMC, Manunuzi, Sheria, Mipango,
Anuwai za Jamii na Utumishi.
Mwezeshaji kutoka NIDA Bw. Josephat Kajonga akielekeza jambo wakati wa Mafunzo hayo. |
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamsikiliza muwezeshaji |
Naulizia nafasi za ajira kwenye jeshi lenu kwa watu tuliokuwa mtaani na sio jkt taratibu zipi nifuate
JibuFuta