Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

24 Julai 2018

Watumishi wa Uhamiaji waanza Mafunzo ya Usimamizi wa Vihatarishi


Baadhi ya Maafisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Makao Makuu wameanza mafunzo ya siku tatu juu ya Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management) katika jengo la Makao Maku ya Idara hiyo Kurasini jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Malyeta ambaye pia ni Mratibu wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Idara hiyo amesema lengo kuu la mafunzo haya ni kuwapa uelewa watumishi  katika Usimamizi wa Vihatarishi kutokana na Muongozo wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Sekta ya Umma (Guidelines for Developing and Implementing Institutiona Risk Management Framework in Public Sector, December 2013) pamoja na Sera ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Idara ya Uhamiaji (Institutional Risk Management Framework and Guide for the Immigration Department, 2016).

 “Kwa muongozo na sera hio tunategemea maafisa wetu watajifunza mambo muhimu sana katika utendaji kazi wao wa kila siku ambayo ni Muundo wa Usimamizi wa Vihatarishi, Wadau wa Usimamizi wa Vihatarishi, Majukumu ya mabingwa wa Vihatarishi, Hatua za Usimamizi wa Vihatarishi, Mgawanyo wa Vihatarishi, rejesta za Viharatishi pamoja na Nyenzo zinazotumika katika Usimamizi wa Vihatarishi’’ aliongeza Mrakibu Msaidizi Malyeta.

Mafunzo haya yanafanyika kwa ushirikiano na wawezeshaji katika Usimamizi wa Vihatarishi kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana Josephat Kajonga ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi na Bi. Lulu Ishengoma ambaye ni Afisa kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi.

Jumla ya Watumishi (askari na kada ya kawaida) 20 wanahudhuria mafunzo haya kutoka vitengo vya Uhasibu, BMC, Manunuzi, Sheria, Mipango, Anuwai za Jamii na Utumishi.

Mwezeshaji kutoka NIDA Bw. Josephat Kajonga akielekeza jambo wakati wa Mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamsikiliza muwezeshaji





Maoni 1 :

  1. Naulizia nafasi za ajira kwenye jeshi lenu kwa watu tuliokuwa mtaani na sio jkt taratibu zipi nifuate

    JibuFuta