Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

25 Mei 2018

Uzinduzi wa Huduma za e-Passport Mkoa wa Dar.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo leo amezindua rasmi Huduma za Utoaji wa Pasipoti ya Kielektronikia katika Mkoa wa Dar es salaam.

Hafla hiyo ya Uzinduzi ambayo ilifanyika katika Viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa, viongozi wa Dini na wananchi kwa ujumla ambapo pamoja na uzinduzi pia walipewa elimu kuhusu pasipoti hio mpya.

Mheshimiwa Injinia Ndikilo alisifu Idara ya Uhamiaji kwa hatua inazochukua katika kuboresha huduma zake kwa wananchi na wageni na aliwataka wananchi kuzitunza pasipoti hizi pindi wanapopatiwa.

”Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, napenda kutoa rai kwa wananchi wote watakaopata Pasipoti hizi za kielektronikia kuhakikisha kwamba wanazitunza vizuri ili zisiangukie mikononi mwa wahalifu. Tambueni ya kwamba, mtu ambaye atapoteza pasipoti hii itamgharimu kulipia Tsh. 500,000/= (kwa atakayepoteza mara ya kwanza) na Tsh. 750,000/= kwa atakayepoteza mara ya pili.” Alisisitiza Mheshimiwa Ndikilo.

Awali Kamishna wa Uhamiaji Pasipoti na Uraia Kamishna Kihinga alieleza kuwa Uzinduzi huu wa leo ni muendelezo ambapo siku kadhaa zilizopita Huduma kama hii ilizinduliwa mkoani Dodoma, ambapo pia Kamishna Kihinga alieleza kuwa hadi kufikia Julai mwaka huu mikoa yote itakuwa tayari imefungwa vifaa vya e-passport.

”Kwa sasa tumeanza kufunga mfumo wa utoaji huduma hizi Mikoani, ambako tumeshaanza kutoa huduma hii katika Jiji la Dodoma, na leo tutaanza kutoa huduma hiyo ya pasipoti katika Ofisi ya Mkoa wa Dar Es Salaam baada ya Mhe. Mgeni rasmi kutuzindulia. Aidha tunatarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu tutakuwa tumekamilisha kufunga Mifumo ya utoaji huduma ya pasipoti mpya Mikoa yote, na hivyo huduma hiyo kutolewa nchi nzima.” Alieleza Kamishna Kihinga.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sophia akiongea na Kamishna wa Pasipoti na Uraia

Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es salaam akimsikiliza kwa makini mkuu wa Wilaya ya Ilala


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum akisalimia na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Ngonyani wakati wa Uzinduzi wa Huduma za e-Passport

Kamishna wa Uhamiaji Pasipoti na Uraia (Kamishna) Kihinga akimpokea mgeni Rasmi Kaimu Mku wa Mkoa wa Dar na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist NdikiloMkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sophia akimsindikiza Mgeni Rasmi

10 Mei 2018

UTARATIBU WA UINGIAJI NA UKAAJI WA WAGENI NCHINI


Sikiliza Mada inayohusu: UTARATIBU WA UINGIAJI NA UKAAJI WA WAGENI NCHINI.
Mtoa Mada ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda kupitia Kituo cha Redio cha Morning Star.