Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo leo
amezindua rasmi Huduma za Utoaji wa Pasipoti ya Kielektronikia katika Mkoa wa
Dar es salaam.
Hafla hiyo ya Uzinduzi
ambayo ilifanyika katika Viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa, viongozi wa Dini na wananchi kwa ujumla ambapo pamoja na uzinduzi pia walipewa elimu kuhusu pasipoti hio
mpya.
Mheshimiwa Injinia
Ndikilo alisifu Idara ya Uhamiaji kwa hatua inazochukua katika kuboresha huduma
zake kwa wananchi na wageni na aliwataka wananchi kuzitunza pasipoti hizi pindi
wanapopatiwa.
”Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, napenda kutoa rai kwa wananchi wote
watakaopata Pasipoti hizi za kielektronikia kuhakikisha kwamba wanazitunza
vizuri ili zisiangukie mikononi mwa wahalifu. Tambueni ya kwamba, mtu ambaye
atapoteza pasipoti hii itamgharimu kulipia Tsh. 500,000/= (kwa atakayepoteza
mara ya kwanza) na Tsh. 750,000/= kwa atakayepoteza mara ya pili.” Alisisitiza Mheshimiwa Ndikilo.
Awali
Kamishna wa Uhamiaji Pasipoti na Uraia Kamishna Kihinga alieleza kuwa Uzinduzi
huu wa leo ni muendelezo ambapo siku kadhaa zilizopita Huduma kama hii
ilizinduliwa mkoani Dodoma, ambapo pia Kamishna Kihinga alieleza kuwa hadi
kufikia Julai mwaka huu mikoa yote itakuwa tayari imefungwa vifaa vya
e-passport.
”Kwa
sasa tumeanza kufunga mfumo wa utoaji huduma hizi Mikoani, ambako tumeshaanza
kutoa huduma hii katika Jiji la Dodoma, na leo tutaanza kutoa huduma hiyo ya
pasipoti katika Ofisi ya Mkoa wa Dar Es Salaam baada ya Mhe. Mgeni rasmi
kutuzindulia. Aidha
tunatarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu tutakuwa
tumekamilisha kufunga Mifumo ya utoaji huduma ya pasipoti mpya Mikoa yote, na
hivyo huduma hiyo kutolewa nchi nzima.” Alieleza Kamishna Kihinga.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sophia akiongea na Kamishna wa Pasipoti na Uraia |
Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es salaam akimsikiliza kwa makini mkuu wa Wilaya ya Ilala |
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum akisalimia na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Ngonyani wakati wa Uzinduzi wa Huduma za e-Passport |
Kamishna wa Uhamiaji Pasipoti na Uraia (Kamishna) Kihinga akimpokea mgeni Rasmi Kaimu Mku wa Mkoa wa Dar na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sophia akimsindikiza Mgeni Rasmi |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni