Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

21 Juni 2018

ELIMU KWA UMMA

ELIMU KWA UMMA:
---------------------------
Je unafahamu kuwa;
Raia wa Tanzania kwa kurithi hawezi kurithisha tena Uraia wake wa Tanzania kwa Mtoto wake aliyezaliwa nje ya Nchi?
Usikose kusikiliza kipindi cha Uraia Wetu kupitia Morning Star FM Radio Leo tarehe 21/06/2017, Saa 4:00 Asubuhi


19 Juni 2018

UZINDUZI WA PASIPOTI ZA KIELEKTRONIKI MKOA WA KAGERA KATIKA PICHA











Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Bukoba Dkt. Methodius Kilaini akisoma sala kabla ya Uzinduzi.











Mkazi wa Bukoba Bwana Jamal Kalumuna akifurahia pasipoti yake mpya ya kielektroniki baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawiro.




Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Kuu la Katoliki Bukoba Mwadhama Desiderius Barthasar Rwoma akikabidhiwa pasipoti yake ya kielektroniki na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawiro.


Sheikh Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Alhaji Kichwabutwa alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Dini waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba.


Kikundi cha Ngoma za Jadi kikitumbuiza

Baadhi ya Maafisa Uhamiaji kutoka Mkoa wa Kagera waliohudhuria Uzinduzi huo



14 Juni 2018

EID EL FITR NJEMA

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji pamoja na Watumishi wote wanawatakia Watanzania wote Eid Elf Fitr Njema.


04 Juni 2018

MATUKIO KATIKA PICHA YA UZINDUZI WA e-PASSPORT MKOA WA KILIMANJARO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira akisalimiana na maafisa na askari wa Uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro kabla ya Uzinduzi wa Pasipoti za kielektroniki mkoani humo mnamo tarehe 30 Mei 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira akipata maelezo ya Utendaji kazi kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akisaini kitabu cha Wageni cha Ofisi ya Uhamiaji Mkoaa wa Kilimanjaro





Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akimpatia pasipoti yake mmoja wa wananchi wa mjini Moshi 

Wanafunzi wa shule ya St. Goreth ya Moshi waliopata pasipoti zao siku ya Uzinduzi




Picha ya pamoja ya Maaafisa na Askari wa Uhamiaji na Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Pasipoti za kielektroniki Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira





Picha ya pamoja baina ya waliopata pasipoti siku ya Uzinduzi na mgeni rasmi katika Uzinduzi huo siku ya tarehe 30 Mei 2018 Mhe. Mama Anna Mghwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya St. Goreth