Hafla ya Uzinduzi wa Huduma
za Pasipoti za Kielekroniki katika ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba
ambayo ilifanyika siku ya tarehe 31/05/2018 ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mhe.
Mohamed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Pemba na viongozi mbali mbali wa Serikali ilifanyika katika Ofisi za
Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba mjini Chakechake.
Mgeni rasmi Mheshimiwa Mohamed Abood katika hotuba yake
alisisitiza sana raia kuleta nyaraka sahihi wanapokuja kuomba pasipoti
ili kurahisisha zoezi la utoaji wa pasipoti hizo, kuwataka kuacha kufoji
nyaraka ili ili kuepuka kutofautiana kwa taarifa muhimu zinazotakiwa.
Pia alikemea utumaji wa mawakala ambao ni mianya ya rushwa, na
watakaogundulika aidha raia au afisa uhamiaji basi wananchi watoe taarifa
kwa Kamishna wa Uhamiaji. Na ikiwa Afisa Uhamiaji anatuhumiwa, Mheshimiwa Abood
alimtaka Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu amsimamishe kazi
mara moja na kupisha uchunguzi juu yake.
Mheshimiwa Abood alimaliza kwa kuwataka wananchi wanaopewa
pasipoti hizo kuzitunza kwani ikipotea gharama ya kuomba inaongezeka na
aliwataka kuzitumia kwa dhumuni husika na sio kuzitupa hovyo.
Hafla hiyo ilimalizika kwa ugawaji wa pasipoti kwa viongozi
mbalimbali waliohudhuria.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba akionesha pasipoti yake |
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Kusini Pemba |
Mhe. Mohamed Abood akipata maekelezo ya hatua za uchuakuaji wa taarifa za mteja kielekroniki |
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maafisa na askari wa Uhamiaji wa ofisi ya Mkoa wa Kusini Pemba |
Mgeni rasmi akiangalia namna ya uchukuaji wa taarifa za kibaiometriki kwa mteja unavyofanyika |
Mwananchi na Mkazi wa Kusini Pemba akikabidhiwa pasipoti yake ya kielektroniki na Mheshimiwa Abood |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni