Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Februari 2022

Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Chafanya Ziara ya Mafunzo Uhamiaji Makao Makuu.

Na. Mwandishi wetu Dodoma, Tanzania

Jeshi la Uhamiaji Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita lilipokea ujumbe wa Wakufunzi 30, na Wanafunzi 43 wa Mataifa mbalimbali, kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kwa ajili ya ziara ya kupatiwa mafunzo ya namna Jeshi la Uhamiaji linavyofanya shughuli zake katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.

Ziara hiyo ya mafunzo ilifanyika katika Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Jijini Dodoma huku ikiongozwa na Brigedia Jenerali Chelestino Msola na kupokelewa na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga ambae alimwakilisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.

Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali ziliwasilishwa na Maafisa kutoka Jeshi la Uhamiaji hususani Pasipoti, Visa za Kielektroniki, Uraia pamoja na mifumo inayotumika katika utoaji wa Pasipoti na visa za kieletroniki.

Aidha, Washiriki wa ziara hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa ipasavyo sanjari na Kutembelea maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma.

Kwa upande wao washiriki walimpongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kwa mafunzo waliyoyapata na kuongeza kuwa, mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu hususani katika kuwahudumia wananchi.

Baada ya kuhitimisha ziara ya mafunzo kwa wanafunzi wa chuo cha Ulinzi wa Taifa  (NDC) katika Makao Makuu ya Jeshi la Uhamiaji Jijini Dodoma ziara hiyo iliendelea tena katika vyombo vingine vya ulinzi na usalama hapa nchini.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga akiongea na baadhi viongozi wa ujumbe kutoka chuo cha Taifa cha Ulinzi wa Taifa (NDC) walipofika Uhamiaji makao makuu kwa ajili ya ziara ya mafunzo



Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC Wakiwa tayari kupatiwa shule ya masuala ya kiuhamiaji

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle akiratibu mafunzo ya masuala ya Uhamiaji wakati wanafunzi kutoka chuo cha ulinzi wa Taifa NDC walipofika kwa ajili ya kujifunza 




Mrakibu wa Uhamiaji Azizi Kilondomara akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa NDC 

Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola Akieleza lengo la ziara yao katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu Dodoma




Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi Jarida la NDC Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga


Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga (Kulia) Aakimkabidhi Kalenda ya Uhamiaji Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola

Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya mwavuli wenye nembo ya NDC Mrakibu wa Uhamiaji Eliud Ikomba ambaye aliwasilisha mada moja wapo ya masuala ya Uhamiaji kwa wanafunzi wa NDC

Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya kofia  yenye nembo ya NDC Mrakibu wa Uhamiaji Azizi Kilondomara ambaye nae aliwasilisha mada moja wapo ya masuala ya Uhamiaji kwa wanafunzi wa NDC

Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kofia yenye nembo ya NDC Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle 


Ziara katika Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma


Muonekano wa maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma

Mtaalamu wa Ujenzi kutoka SUMAJKT akitoa maelezo ya ujenzi


Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ulinzi wa Taifa NDC  wakifurahia jambo


(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

27 Februari 2022

JESHI LA UHAMIAJI WILAYA YA NGORONGORO LAZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI

Na. Paul Dudui, LOLIONDO, NGORONGORO

Suala la mabadiliko ya tabia ya nchi (Climate change) limekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mbalimbali Duniani kote, ambapo sasa Dunia ina haha kupambana na Mabadiliko haya ambayo yameathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya watu na viumbe hai wengine, Mabadiliko ya tabia nchi yanaletwa pia na aina ya maisha ya binadamu, ambapo watu wengi hupenda kuharibu mazingira yanayo wazunguka jambo ambalo limesababisha hali mbaya ya hewa ambayo inazidi kuathiri ustawi wa watu na viumbe hai wengine

Kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro na hasa eneo la Loliondo ambalo ni eneo la nyanda za juu ambalo kihistoria lilikuwa sehemu ya baridi kali kutokana na uoto wa asili uliokuwepo wakati huo, hata hivyo hali imebadilika sana na kutokana aina ya maisha ya watu ambayo yameharibu mazingira ya asili na kusababisha Mabadiliko makubwa sana ya tabia ya nchi.

Kutokana na hali hii Jeshi la Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro limeibuka na kampeni kabambe ya kuhamasisha upandaji miti kama hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuhifadhi mazingira ya Mji mdogo wa Loliondo, Kikosi hiki cha Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro kikiongozwa na Afisa Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro Mrakibu Lidya Angumbwike kimeendesha kampeni hiyo kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya mji wa Loliondo ambapo hadi kufikia leo ambapo ilikuwa siku rasmi ya kupanda miti Kiwilaya kimeshapanda miti zaidi ya 1200

Katika siku hii ya kupanda miti kiwilaya iliyoasisiwa na Jeshi la Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro, Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Mheshimiwa Mwalimu Raymond Mangwala, ambaye aliwakilishwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ngorongoro SSP Peter Lusesa, kutokana na Mkuu wa wilaya kuwa na majukumu mengine ya kikazi

Hafla ya upandaji miti Kiwilaya, iliyoasisiwa na Jeshi la Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro, ilifanyika katika vya Ofisi za Uhamiaji Wilaya na kuhudhuriwa na; Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Viongozi wa Dini, Watumishi wa Halmashauri na taasisi za umma wakiwemo TARURA, NMB, PCCB, Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Viongozi wa kijamii na wananchi wa mji mdogo wa Loliondo wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji, Bwana Benezeth Bwikizu.

Akizungumza mara baada ya shughuli ya upandaji miti, Mgeni rasmi amesema kazi ya upandaji miti ni muhimu sana katika kupambana na  mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanazidi kuathiri Duniani, lakini pia kupanda miti kunaongeza uwezekano wa kutunza mazingira yetu tunayoishi, kwa kuwa miti ni uhai wetu.

Nae Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Loliondo, bwana Benezeth Bwikizu, Akizungumza katika hafla hiyo, amelishukuru Jeshi la Uhamiaji kwa kubuni na kutekeza zoezi hilo ambapo amesema wao kama Mamlaka ya Mji wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa endelevu, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaelekeza wananchi wote wa mji mdogo wa Loliondo kuhakikisha kila mtu nyumbani kwake na maeneo yake ya kazi ana panda miti mitano kila mwaka ili kutokomeza upepo mkali uliopo katika maeneo ya mji wa Loliondo, Mtendaji huyo ameenda mbali zaidi ambapo alisema wao kama Mamlaka ya Mji mdogo wa Loliondo, itakuja na kampeni yenye ujumbe unaosema "Tokomeza Upepo Wasso, ambapo amesema kampeni hii iliyoasisiwa Uhamiaji, imekuwa kichocheo kikubwa sana.

Nao viongozi wa dini wakiongozwa na Mchungaji Wachira wa GCCT Loliondo, wamesema kampeni hii ni mhimu sana kuungwa mkono na kila mtu ambaye ana hofu ya Mungu kwa kuwa Mungu pia anapenda pia kuwa na mazingira mazuri, Viongozi hao wamesema watawasisitiza waumini wao katika maeneo yao ya Ibada (Kanisani na Misikitini) kuhakikisha kuwa ujumbe huu unafika kwa jamii ili kampeni hii iwe endelevu na itakayoleta matokeo makubwa

Awali akitoa taarifa ya kampeni hiyo Kamanda wa Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro, SI. Lidya Angumbwike amesema kauli mbiu ya Uhamiaji katika shughuli hiyo ni; "Uhamiaji na Maendeleo, Tunza Mazingira kwa Maendeleo ya Vizazi vya Sasa na Vijavyo"

Kwa upande wa wananchi wa Loliondo waliohudhuria katika hafla hiyo wamesema, wao wanalishukuru Jeshi la Uhamiaji Wilaya kwa kuwakumbusha wajibu wao na kwamba kwao kampeni hiyo itakuwa endelevu, aidha wananchi wamempongeza Afisa Uhamiaji Wilaya kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Loliondo ambapo wameahidi kuwa miti iyopandwa watailinda ili iweze kusitawi na kukua.

Mwandishi wa Makala hii naye anatumia makala hii kulipongeza Jeshi la Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro kwa namna ambavyo limejitikita katika kutoa elimu ya Uraia na Mazingira, kimsingi Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro pamoja na kufanya shughuli zao katika mazingira magumu lakini bado wamekuwa wabunifu katika upelekaji ujumbe kwa umma.

"Tunza Mazingira yakutunze"

HABARI PICHA NA MATUKIO

Afisa Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro Mrakibu Lidya Angumbwike akipanda mti

Maafisa na Askari wa Uhamiaji Ngorongoro wakipanda miti

Baadhi ya viongozi na wananchi Wilayani Ngorongoro walioshiriki zoezi la upandaji miti


19 Februari 2022

CGI Dkt. Anna Makakala akutana na Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa Nchi hiyo

Na. Konstebo Amani Mbwaga, Dar es Salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala jana tarehe 18 Februari 2022 amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari na kufanya nao Mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji nchini Qatar.

Mazungumzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Aidha baada ya kumaliza mazungumzo hayo ya masuala ya Uhamiaji wageni hao walipata pia fursa ya kukutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo yaliwahusisha viongozi wa Wizara akiwemo Waziri na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizarani, sanjari na Uhamiaji ikiongozwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akiambatana na Kamishna wa Huduma za Sheria Novaita Mrosso.

Mazungumzo hayo yalilenga kuhusu kuendeleza Uhusiano mkubwa uliopo baina ya Tanzania na Qatar lakini pia kushirikiana katika masuala ya ajira kwa vijana nchini Qatar, Utalii, Uwekezaji na masuala ya Ki-Uhamiaji.

Akifungua mazungumzo hayo baina ya Nchi mbili Waziri Joyce Ndalichako aliwashukuru na kuwapongeza Qatar kwa kupata fursa ya kuandaaa mashindano ya Kombe la Dunia sanjari na kuikaribisha Tanzania kutumia fursa hiyo nchini Qatar kwa faida ya nchi zote mbili Kiuchumi, Kisiasa, Kiutamaduni na Kijamii.

 #Kaziiendelee #TanzaniaQatar2022

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akifanya Mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.



 Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali  (wa kwanza Kulia) akiwa na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari wakizungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Hayupo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo yakiendelea


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja kulia kwake ni na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali na kushoto kwake ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari, akifuatiwa na Kamishna wa Huduma za Sheria Uhamiaji Tanzania Novaita Mrosso baada ya Mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akimpa zawadi (souvenir) Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari baada ya kufanya mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akikipokea zawadi (souvenir) kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari baada ya kufanya mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam.








Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali


Mazungumzo na Waziri Ndalichako yakiendelea





Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Aliyesimama) akijitambulisha katika kikao cha Mazungumzo baina ya Nchi ya Qatar na Tanzania kilichofanyika Serena Hotel Jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akizungumza



 Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini Qatar Mohammed Ahmed al Dosari akisikiliza kwa makini mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji, Ajira Utalii na Uwekezaji Jijini Dar es Salaam.






Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini Qatar Mohammed Ahmed al Dosari akisikiliza kwa makini mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji, Ajira Utalii na Uwekezaji Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akimpatia zawadi ((souvenir)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akimpatia zawadi ((souvenir)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akipokea zawadi ((souvenir) kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.



   ( Picha zote na Konstebo Amani Mbwaga )