Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

19 Februari 2022

CGI Dkt. Anna Makakala akutana na Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa Nchi hiyo

Na. Konstebo Amani Mbwaga, Dar es Salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala jana tarehe 18 Februari 2022 amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari na kufanya nao Mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji nchini Qatar.

Mazungumzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Aidha baada ya kumaliza mazungumzo hayo ya masuala ya Uhamiaji wageni hao walipata pia fursa ya kukutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo yaliwahusisha viongozi wa Wizara akiwemo Waziri na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizarani, sanjari na Uhamiaji ikiongozwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akiambatana na Kamishna wa Huduma za Sheria Novaita Mrosso.

Mazungumzo hayo yalilenga kuhusu kuendeleza Uhusiano mkubwa uliopo baina ya Tanzania na Qatar lakini pia kushirikiana katika masuala ya ajira kwa vijana nchini Qatar, Utalii, Uwekezaji na masuala ya Ki-Uhamiaji.

Akifungua mazungumzo hayo baina ya Nchi mbili Waziri Joyce Ndalichako aliwashukuru na kuwapongeza Qatar kwa kupata fursa ya kuandaaa mashindano ya Kombe la Dunia sanjari na kuikaribisha Tanzania kutumia fursa hiyo nchini Qatar kwa faida ya nchi zote mbili Kiuchumi, Kisiasa, Kiutamaduni na Kijamii.

 #Kaziiendelee #TanzaniaQatar2022

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akifanya Mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali  (wa kwanza Kulia) akiwa na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari wakizungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Hayupo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo yakiendelea


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja kulia kwake ni na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi wa nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali na kushoto kwake ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari, akifuatiwa na Kamishna wa Huduma za Sheria Uhamiaji Tanzania Novaita Mrosso baada ya Mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji katika Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akimpa zawadi (souvenir) Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari baada ya kufanya mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akikipokea zawadi (souvenir) kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wa Qatar Mohammed Ahmed al Dosari baada ya kufanya mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali


Mazungumzo na Waziri Ndalichako yakiendelea

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Aliyesimama) akijitambulisha katika kikao cha Mazungumzo baina ya Nchi ya Qatar na Tanzania kilichofanyika Serena Hotel Jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akizungumza Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini Qatar Mohammed Ahmed al Dosari akisikiliza kwa makini mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji, Ajira Utalii na Uwekezaji Jijini Dar es Salaam.


Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini Qatar Mohammed Ahmed al Dosari akisikiliza kwa makini mazungmzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhamiaji, Ajira Utalii na Uwekezaji Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akimpatia zawadi ((souvenir)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akimpatia zawadi ((souvenir)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Bw. Mohamed Hassan al Obaidali akipokea zawadi ((souvenir) kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel uliopo Jijini Dar es Salaam.   ( Picha zote na Konstebo Amani Mbwaga )


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni