Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Machi 2020

MSEMAJI Mpya wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Atambulishwa Rasmi ITV na Redio One

Dar es salaam, Tanzania 
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle mapema leo hii ametambulishwa rasmi katika studio za  ITV, East Afrika Redio Na Redio One zilizopo Mikocheni Jijini Dar es salaam 

Tukio hilo limeongozwa na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda ambaye amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuongozwa na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari wa ITV na Redio  huku akiwahakikishia ushirikiano wa kutosha kama aliokuwa nao Msemaji Mkuu aliyepita.

Ikumbukwe kuwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko madogo ya Uongozi kwa Wakuu wa Vitengo katika Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma mapema wiki hii.


Katika Mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uraia, Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle ameteuliwa kuwa Msemaji wa Idara ya Uhamiaji na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano.

Aidha, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Makakala pia amemteua Mrakibu wa Uhamiaji Lucy Ansyline Nyaki kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uraia. Kabla ya uteuzi huo, Nyaki alikuwa Afisa katika Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Uhamiaji.

Viongozi walioteuliwa katika nyadhifa hizo mpya wataanza kutekeleza rasmi majukumu yao kuanzia kesho tarehe 01 Aprili, 2020.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda akitoa neno la shukurani kwa Kampuni ya IPP Media kwa ushirikiano waliompa wakati wote wa uongozi wake
 

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle aliyeteuliwa hivi karibuni, mapema leo hii ametambulishwa rasmi katika studio za  ITV, East Afrika Redio na Redio One zilizopo Mikocheni Jijini Dar es salaam


Msemaji Mpya wa Uhamiaji na Aliyepita wakiwa katika Moja ya redio za IPP Media, Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (kulia) akibadilishana mawasiliano na waandishi wa Habari wa ITV


Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (Kushoto) akiagana na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa  kwa salamu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoshikana mikono
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda akiagana na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa  kwa salamu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoshikana mikono
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

16 Machi 2020

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATEMBELEA UJENZI WA JENGO LA UHAMIAJI MAKAO MAKUU

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Victor Mwambalaswa imetembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa  jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma leo Jumatatu Machi 16, 2020.

Kamati hiyo ambayo ilipokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene , Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari  Masoud Sururu, Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha) Edward Chogero pamoja na Maafisa Uhamiaji Waandamizi katika eneo la ujenzi wa mradi huo.

Mhandisi Kanali Zabron Mahenge ambaye ni Meneja Mradi kutoka Jeshi la Kujenga Taifa aliieleza Kamati hiyo kuwa ujenzi unaendelea vizuri pamoja na kuwepo changamoto ndogo ndogo na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya Ujenzi huo, Mhandisi wa Mradi David Pallangyo alisema hadi sasa ujenzi umefikia hatua nzuri ambapo sakafu ya ghorofa ya tatu imekamilika kwa 60% na ujenzi utakamilika kwa muda uliopangwa.

Mwenyekiti wa Kamati  ya Bunge  Mhe.Mwambalaswa alimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kamishna Jenerali pamoja na wahandisi  kwa usimamizi mzuri ujenzi wa Jengo hilo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili ujenzi ukamilike kama ilivyopangwa.

Nae Mjumbe wa Kamati hiyo ya Bunge Mhe. Almas Maige  hakusita kutoa pongezi kwa  Wizara ya mambo ya Ndani na Idara ya Uhamiaji kwa ujenzi wa jengo hilo la Makao Makuu ambalo ni kubwa na la kisasa pindi litakapokamilika.

Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma lenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 20 unaojengwa na  Suma JKT unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya  Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma ukiendelea

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akimlaki Katibu Mkuu Mambo ya Ndani Mh. Christopher Kadio alipowasili katika eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya uhamiaji jijini Dodoma leo tarehe 16 Machi 2020.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu akiongea na Katibu Mkuu mambo ya Ndani ya Nchi

Katika kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona, Katibu Mkuu akinawa mikono kwenye eneo la ujenzi

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akinawa mikono yake ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la ujenzi wa ofisi za Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. George Simbachawene akilakiwa na Makamishna wa Uhamiaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji 

Waziri Simabachawene akinawa mikono yake kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona
Waziri Simbachawene akiongea na Wahandisi na mafundi wanaojenga jengo la Uhamiaji Makao Makuu Dodoma


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mhe. Mwambalaswa akishuka katika basi lililowabeba wajumbe wa Kamati hiyo walipowasili katika eneo la Ujenzi 

Wanakamati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakinawa mikono yao 


Mh. Vuai Nahodha akinawa mikono yake kujikinga na Corona wakati walipowasili eneo la Ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge akioneshwa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Uhamiaji Makao Makuu na Waziri Simbachawene

Mwenyekiti wa Kamati na Wajumbe wakisoma taarifa ya Maendeleo  ya Ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji
Mjumbe wa Kamati Mhe. Almas Maige akichangia jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati akitoa neno alke wakati wa ziara ya kamati yake


Ukaguzi wa ujenzi ukiongozwa na Wahandisi David Pallangyo na Kanali MahengeWajumbe wakikagua sakafu ya chini ya jengo (Basement) katika jengo la Uhamiaji Makao Makuu

Wajumbe wa kamati wakikagua ujenzi wa sakafu ya ghorofa ya tatu unaondelea

Mh. Almas Maige akikagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa sakafu ya ghorofa ya tatu

Sehemu ya Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge wakishuka ngazi za Jengo la Uhamiaji Makao Makuu linaloendelea kujengwa jijini DodomaKamishna Jenerali wa Uhamiaji akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji jijini DodomaKamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sululu na Kamishna wa Uhamiaji Edward Chogero (Utawala na Fedha) ni miongoni mwa waliohudhuria ukaguzi huo