Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Machi 2020

MSEMAJI Mpya wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Atambulishwa Rasmi ITV na Redio One

Dar es salaam, Tanzania 
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle mapema leo hii ametambulishwa rasmi katika studio za  ITV, East Afrika Redio Na Redio One zilizopo Mikocheni Jijini Dar es salaam 

Tukio hilo limeongozwa na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda ambaye amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuongozwa na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari wa ITV na Redio  huku akiwahakikishia ushirikiano wa kutosha kama aliokuwa nao Msemaji Mkuu aliyepita.

Ikumbukwe kuwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko madogo ya Uongozi kwa Wakuu wa Vitengo katika Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma mapema wiki hii.


Katika Mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uraia, Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle ameteuliwa kuwa Msemaji wa Idara ya Uhamiaji na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano.

Aidha, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Makakala pia amemteua Mrakibu wa Uhamiaji Lucy Ansyline Nyaki kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uraia. Kabla ya uteuzi huo, Nyaki alikuwa Afisa katika Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Uhamiaji.

Viongozi walioteuliwa katika nyadhifa hizo mpya wataanza kutekeleza rasmi majukumu yao kuanzia kesho tarehe 01 Aprili, 2020.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda akitoa neno la shukurani kwa Kampuni ya IPP Media kwa ushirikiano waliompa wakati wote wa uongozi wake
 

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle aliyeteuliwa hivi karibuni, mapema leo hii ametambulishwa rasmi katika studio za  ITV, East Afrika Redio na Redio One zilizopo Mikocheni Jijini Dar es salaam


Msemaji Mpya wa Uhamiaji na Aliyepita wakiwa katika Moja ya redio za IPP Media, Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (kulia) akibadilishana mawasiliano na waandishi wa Habari wa ITV


Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (Kushoto) akiagana na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa  kwa salamu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoshikana mikono
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda akiagana na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa  kwa salamu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoshikana mikono
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni