Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

15 Machi 2020

Uhamiaji Tanzania FT Yapania Kupanda Ligi kuu Zanzibar

Timu yetu ya mpira wa Miguu ya uhamiaji (Uhamiaji Football Team) inayoshoriki ligi daraja la kwanza Visiwani Zanzibar ipo mbioni kuwania kupanda ligi kuu Visiwani Zanzibar.

Hii inathibishwa na kua katika mwenendo mzuri wa timu.

Uhamiaji Tanzania FT ipo nafasi ya nne ikiwa na alama 27 nyuma ya Black Sailors ambayo inashika usukani wa ligi yenye alama 34 ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Timu ya Uhamiaji ina wachezaji mchanganyiko yaani askari wa Uhamiaji na raia hali inayopelekea timu hii kua imara zaidi na kuzidi kuchanja mbuga kila leo kwa malengo ya kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa  msimu ujao wa mwaka 2020/2021.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Pichani ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu akikabidhi Jezi na vifaa mbali  vya michezo kwa wachezaji na viongozi wa Timu ya Uhamiaji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Pichani ni katibu mkuu wa Uhamiaji football team ASI. Saleh akimtilisha saini wa mkataba Kocha m Bw. Kijo tayari kuwatumikia wana idara ya Uhamiaji 


Pichani ni Mkaguzi wa Uhamiaji Abdallah Makunja alipowatembelea wachezaji na kupata kuabadilishana mawazo juu ya kuimarisha timu, hapa akiwa wachezaji Askari waIdara 
Benchi la Ufundi likifuatilia kwa makini mchezo unaoendalea (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Zanzibar)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni