Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James Mwanjotile amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara yaani Masasi, Newala, Nanyumbu na Tandahimba.
Lengo
kuu la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiutendaji katika
wilaya hizo na Mkoa kwa ujumla.
Akizungumza
na Maafisa, Askari na watumishi raia wa Uhamiaji katika Wilaya hizo, Kamishna
Msaidizi Mwanjotile, amesisitiza kuhakikisha kuwa wanatunza vifaa vyote vya Ofisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi wakizingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali.
Aidha,
amewakumbusha Maafisa Uhamiaji Wilaya kuendelea kutoa elimu kwa umma ambapo,
Mkoa wa Mtwara tayari umeshaanza kuandaa programu maalum za Elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa
Umma kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi hususani katika kipindi hiki cha
kuelekea Uchaguzi Mkuu, na kuhakikisha wanashughulikia changamoto za uraia zitakazo jitokeza wakati wa kipindi cha
uchaguzi, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt.
Anna Peter Makakala alilolitoa hivi karibuni Jijini Dodoma.
Vilevile
Kamishna Msaidizi Mwanjotile ametoa wito kwa Maafisa Uhamiaji Wilaya wote wa
Mkoa huo kuhakikisha kuwa wageni wote wanaoishi katika maeneo yao wanafuata
sheria, sanjari na kusisitiza kuongeza udhibiti wa uingiaji na utokaji wa wageni na
raia wa Tanzania katika mipaka yote ya Mkoa huo kwa kuimairisha doria na misako
ya wahamiaji haramu kote nchini ili kuhakikisha kuwa nchi inabaki salama na wahamiaji
haramu hawanufaiki na rasilimali zetu.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James Mwanjotile akiwa katika moja ya Ofisi ya Uhamiaji Wilaya wakati wa ziara yake. |
Baadhi ya vitendea kazi vikishushwa katika moja ya Wilaya za Mkoa wa Mtwara (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni