Dar es salaam, Tanzania
Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala mapema leo hii katika Ofisi ndogo za Makao Makuu
ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam amepokea ugeni kutoka Ubalozi wa
Japani nchini Tanzania na kufanya mazungumzo.
Ugeni huo umekuja na ujumbe wa kuwasilisha hati mpya za kusafiria (Japanese Travel Documents Model 2020) zilizoboreshwa ambazo zinatumika hivi sasa nchini Japani ikiwa na lengo la kusambaza toleo lao jipya la Pasipoti kwa nchi mbalimbali duniani ili ziweze kutambulika pale raia wao wanapoingia nchini, na huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa kila nchi inapozindua pasipoti yake mpya basi lazima ipekeleka mfano wa hati hizo mpya (Travel Documents Model) katika Mataifa mbalimbali ili ziweze kujulikana na kutumika Kimataifa.
Dkt. Makakala ameishukuru serikali ya Japani kwa kuendeleza Mahusiano mazuri yaliyopo hususani katika masuala ya kiuhamiaji na kusaidiana katika kutatua changamoto mbalimbali za kiuhamiaji zinazoweza kujitokeza kwa watanzania na raia wa Japani ikiwa sanjari na utekelezaji wa mfumo wa Uhamiaji Mtandao.
Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ni Mfumo unaounganisha mifumo yote ya utoaji huduma kwa njia za kielektroniki, hivyo kupitia Uhamiaji Mtandao huduma mbalimbali za kiuhamiaji kama vile Pasipoti, Vibali, Visa, pamoja na usimamizi na udhibiti wa mipaka kielekroniki hutolewa.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Muonekano wa Hati mpya za kusafiria (Japanese Travel Documents Model 2020) zilizoboreshwa ambazo zinatumika hivi sasa nchini Japani |
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala (Kulia) akimsikiliza Mwakilishi wa Ubalozi wa Japani Nchi Tanzania akitoa Maelezo ya Pasipoti mpya ya Japani |
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala (Kulia) akioneshwa baadhi ya nyaraka zinazothibitisha ubora wa viwango vya Kimataifa katika Pasipoti mpya ya Japani |
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala (Kulia) akimkabidhi Jarida la Uhamiaji Mwakilishi wa Ubalozi wa Japani Nchini Tanzania. |
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala (Kulia) akibadilishana Mawasiliano na wawakilishi wa Ubalozi wa Japani baada ya kumaliza maungumzo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni