Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

05 Machi 2020

KATIBU MKUU ALIPOTEMBELEA MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Christopher Kadio akiingia katika ofisi za Makao makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa Idara hiyo leo tarehe 5 Machi 2020.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu WMNN Ndugu Christopher Kadio alipofanya ziara ya kikazi katika makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma. 


Awali Katibu Mkuu Ndugu Kadio alifanya kikao cha ndani na Makamishna wa Uhamiaji katika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma.Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Makakala akimkaribisha Katibu Mkuu kuongea na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma

Baadhi ya Maafisa Uhamiaji wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Katibu Mkuu
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu akifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu WMNN leo taerehe 05 Machi 2020.

Katibu Mkuu WMNN Ndugu Kadio akiandika maoni ya mmoja wa wachangiaji alipokutana na watumishi wa Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma.

Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji Dereva Mwandamizi Beno Kereti akitoa maoni wakati wa kikao na Katibu Mkuu WMNN

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar akitoa neno la shukrani kwa ujio wa Katibu Mkuu WMNN mara baada ya kuongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia katika ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni