Akizungumza
na Maafisa na Askari wa Uhamiaji, Dkt. Makakala amewata Maafisa Uhamiaji Mikoa
wote nchini kuandaa programu maalum za Elimu ya Uraia kwa Umma kwa kushirikiana
na Tume ya Uchaguzi hususan katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
"Nchi yetu Mwaka huu inafanya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hivyo ni rai yangu kwa Maafisa
Uhamiaji Mikoa kushirikiana vyema na Tume ya Uchaguzi kwa kutoa elimu ya uraia
kwa wananchi na kushughulikia changamoto za uraia zitakazo jitokeza wakati wa
kipindi cha uchaguzi na kuhakikisha kuwa wanazipatia majibu kwa wakati" amesema Dkt. Makakala.
Vilevile
Dkt. Makakala ametoa wito kwa Maafisa
Uhamiaji Mikoa hao kuhakikisha kuwa
Wageni wote wanaoishi katika maeneo yao wanaishi kwa kufuata sheria.
Aidha,
Maafisa Uhamiaji wote wametakiwa kuimairisha Doria na Misako ya Wahamiaji
haramu kote nchini ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inabakia kuwa salama na
Wahamiaji haramu hawanufaiki na rasilimali zetu.
Kwa
Upande wake Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Divisheni ya Vibali vya Ukaazi,
Visa na Pasi, Mary Palmer (ndc) amewataka raia wa kigeni wote wanaoishi nchini
kuhakikisha kuwa wana vibali vya Ukaazi.
Kamishna
Palmer amesisitiza kuwa wageni wanaohitaji kuingia na kuishi nchini kwa
madhumuni mbalimbali wanaweza kufanya maombi, kulipia na kupokea nakala za
vibali vyao kwa njia ya mtandao.
Awali
akitoa taarifa ya Utendaji kazi ya Mkoa, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Abdallah Katimba ameeleza kuwa Mkoa wa Dodoma
umeimarisha Doria na Misako dhidi ya Wahamiaji haramu, na pia Mkoa umejipanga
vyema kutoa Elimu ya Uraia kwa Watanzania.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiongea na mmoja wa wateja wa huduma za Uhamiaji katika ofisi ya uhamiaji mkoa Dodoma. |
Baadhi ya Askari na Maafisa wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji alipofanya ziara katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni