Ofisi ya Uhamiaji
Mkoa wa Iringa imetekeleza agizo la Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna
Peter Makakala alilolitoa mapema wiki hii akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani
Dodoma kwa Maafisa Uhamiaji Mikoa yote nchini kutoa elimu ya Uhamiaji na Uraia
kwa watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020.
Akizungumzia kuhusu
Utekelezaji huo, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji
Agness Luziga amesema Maafisa na Askari wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa wanatembelea
Maeneo mbalimbali Mkoani humo kwa ushirikiano na vyombo vya habari vikiwemo
Vituo vya Radio, Televisheni na Mitandao ya Kijamii kutoa elimu ya Uhamiaji na
Uraia hasa kuelekea kipindi hiki muhimu cha Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani.
Kwa kushirikiana na
Kituo cha Redio Furaha Fm 96.7 kilichopo katika Manispaa ya Iringa, wametoa
elimu ya Uraia kwa Wananchi wa Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Kupitia Kipindi
hicho Wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi kuhusu
huduma za Uhamiaji na Uraia.
Afisa Uhamiaji Mkoa
huyo amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na litashirikisha Viongozi wa
Serikali za Mitaa, Tume ya Uchaguzi pamoja na Jamii kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni