Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Divisheni ya Vibali vya
Ukaazi, Pasi na Visa, Mary Palmer (ndc) ameongoza
Ujumbe wa Mabalozi 03 katika Mafunzo ya huduma mbalimbali za kiuhamiaji
zinazotolewa katika Balozi za Tanzania Nje ya Nchi.
Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria mafunzo hayo ni Maj.
Gen. Jacob Kingu, Kamishna Jenerali (Mstaafu) wa Magereza Phaustine Kasike na Dkt. John Simbachawene ambao wameteuliwa hivi karibuni na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli.
Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali ziliweza
kuwasilishwa na Maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji hususani Pasipoti, Visa za
kielektroniki, pamoja na Mifumo inayotumika katika utoaji wa Pasipoti na Visa za
kieletroniki.
Aidha, Waheshimiwa Mabalozi walipata fursa ya kuuliza
maswali na kujibiwa ipasavyo na watoa mada sanjari na kufurahishwa na namna
mifumo mbalimbali ya Uhamiaji inavyofanya kazi na kurahisisha utoaji wa huduma za uhamiaji
kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake Balozi Mteule wa Tanzania Meja
Jenerali Jacob Kingu kwa niaba ya mabalozi wenzake alimshukuru na Kumpongeza
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa mafunzo waliyoyapata.
Pia ameongeza kuwa, mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa
kwenda kufanya kazi kwa ufanisi hususani katika kuwahudumia Watanzania waishio
nje ya nchi na wageni wanaoingia hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali
ikiwemo utalii, matembezi, Biashara na uwekezaji.
Mafunzo hayo Yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam na ni muendelezo wa Elimu ya Uhamiaji na
Uraia inayotolewa na Idara ya Uhamiaji kwa Makundi mbalimbali ikiwemo
Wanadiplomasia.
|
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Divisheni ya Vibali vya Ukaazi, Pasi na Visa, Mary Palmer (ndc) akitoa utangulizi wa Mafunzo kwa Mabalozi Wateule. |
|
Balozi Mteule Maj. Gen. Jacob Kingu, akisikiliza kwa makini elimu anayopatiwa kutoka kwa Maafisa Uhamiaji |
|
Mkaguzi wa Uhamiaji Gerald Kawishe akifundisha somo la Uraia na Pasipoti kwa Mabalozi wateule |
|
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Godbless Swai akifundisha somo la Vibali vya Ukaazi na Visa kwa Mabalozi wateule (hawapo pichani) |
|
Mabalozi wateule wakisoma kwa vitendo namna ya kukagua nyaraka mbalimbali za Kiuhamiaji |
|
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Ritha Muumba akifundisha Huduma za kibalozi (Consular Services) kwa Mabalozi wateule |
|
Afisa TEHAMA Mwandamizi Rodern Mtulo Akisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa mabalozi wateule baada ya kupata mafunzo ya Huduma za Kiuhamiaji |
|
Picha ya Pamoja baada ya kumaliza Mafunzo |
|
Mabalozi Wateule wakiagana baada ya kumaliza mafunzo katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini Dar es salaam (Picha na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni