Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Christopher Kadio amefanya ziara ya Kikazi Ofisi
ya Uhamiaji Makao Makuu na kuzungumza na Menejimenti, Maafisa, Askari na
Watumishi raia wa Uhamiaji alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji -
Dodoma, kwa lengo la kuona na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinaikabili Idara
ya Uhamiaji na kuomba ushirikiano wa kutatua kwa pamoja.
Akizungumza na Watumishi hao,
Katibu Mkuu Kadio amesisitiza utendaji kazi wenye kuzingatia weledi, nidhamu na
unyenyekevu hasa wakati wa kupokea mrejesho wa huduma za Uhamiaji hususan
kupitia malalamiko ama ukosoaji wa namna yoyote toka kwa watu Wananchi.
"Kupokea
malalamiko na kuyafanyia kazi ni njia nzuri ya kutunza taswira ya taasisi na
ama kulinda hadhi ya Idara yenu” amesisitiza
Aidha, Katibu Mkuu amewataka
watumishi hao kutoa maoni yao na ushauri kwa lengo kuboresha ufanisi wa
Utendaji kazi.
Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi amesisitiza kuwa endapo Idara itafanikiwa kuzitatua
changamoto zinazioikabili itakuwa ni Mafanikio kwa Wizara na Serikali kwa
ujumla.
Pia Katibu Mkuu Kadio
ameipongeza Idara kwa kuboresha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma za Paspoti
na kuwaasa kuwa kazi kubwa waliyonayo ni kulinda mafanikio hayo na kuendelea
kuboresha zaidi ya ubora uliopo sasa.
Akihitimisha mazungumzo yake
Ndugu Kadio ameahidi kukutana na watumishi mbalimbali walio chini ya Wizara na
taasisi zake mara nyingi iwezekanavyo kwa lengo na kutatua changamoto
zinazojitokeza na kuboresha zilizotatuliwa na kuongeza ubora zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni