Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa mapema wiki hii imeendelea kutekeleza maelekezo ya Kamishina Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kwa kutoa elimu ya Ki-uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali ya habari
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACI Agnes Luziga ameeleza kwamba Mkoa huo sasa umejiwekea mpango mkakati wa kuendelea kutoa elimu kwa umma mara kwa mara katika masuala mbalimbali ya Ki-uhamiaji
Kupitia 96.7 Radio Furaha Fm iliyopo Iringa mjini, wananchi wameweza kupata elimu ya aina za pasipoti na hati za kusafiria, ambapo Konstebo wa Uhamiaji Richard Nzagi pamoja na Konstebo Mariam Simba kutoka kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa wameelezea kwa kina vigezo vya kupata hati hizo za kusafiria ambazo ni pasipoti ya kawaida (Ordinary Passport), pasipoti ya utumishi(Service Passport), pasipoti ya kidiplomasia (Diplomatic Passport), hati ya utambulisho, hati ya kusafiria ya dharula na hati ya kusafiria ya mkataba wa Geneva.
Aidha wameeleza pia dhana ya Uhamiaji Mtandao ambapo ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ya ki-uhamiaji ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za ki-uhamiaji, huduma hizo ni e-Visa, e-Resident Permit, e-Passport, na e-Border Management.
Mbali na hayo walitoa pia elimu ya masuala ya uhamiaji haramu na madhara yake kwa ulinzi na usalama wa nchi yetu sanjari na kusisitiza kwamba suala la la ulinzi na usalama wa nchi ni jukumu la kila mtanzania hasa mzalendo.
#Zuia uhamiaji haramu.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Konstebo wa Uhamiaji Richard Nzagi pamoja na Konstebo Mariam Simba kutoka kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa wakitoa elimu kwa umma kwa njia ya redio mkoani Iringa |
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni