Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala mapema wiki hii alihudhuria ibada ya mwisho na mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, katika uwanja wa Magufuli na makaburi ya familia yaliyopo Chato, Mkoani Geita.
Majira ya saa 10:50 jioni jeneza lenye mwili wa Hayati Magufuli lilishushwa kaburini na kufuatiwa na tukio la ndugu, jamaa na marafiki kuweka mchanga.
Hayati Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 61.
Shughuli ya mazishi imeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, mke wa marehemu Mama Janeth Magufuli, marais wastaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, viongozi wa dini na siasa.
Mbali na hao shughuli hiyo pia imeshuhudiwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafamilia, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makamishna wa Uhamiaji, wasanii pamoja na baadhi ya wakazi wa Chato na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Shughuli ya maziko ilifanyika Kijiji cha Mlimani wilayani Chato Mkoa wa Geita katika makaburi ya familia ilihusisha watu wachache wakiwemo viongozi wa Serikali, wastaafu na familia yake.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake kwa wafiwa na wanachi kwa ujumla wakati wa Ibada ya mwisho ya mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato Mkoani Geita |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Katikati) akiwasili katika eneo la mazishi
|
Makamishna wa Uhamiaji, maafisa, askari na wanachi wengine wakishiriki ibada ya mwisho ya mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato Mkoani Geita |
|
Makamishna wa Uhamiaji, maafisa, askari na wanachi wengine wakishiriki ibada ya mwisho ya mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli chato mkoani Geita |
|
Viongozi wa dini |
|
Makamishna wa Uhamiaji, maafisa, askari na wanachi wengine wakishiriki ibada ya mwisho ya mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala (Katikati) akiwasili katika eneo la mazishi |
|
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi (kushoto) Mhe. George Simbachawene akiwasili katika eneo la mazishi |
|
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoka eneo la mazishi |
|
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu Dodoma) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni