Dar es salaam
Idara ya Uhamiaji Tanzania imeibuka na Ushindi wa tuzo mbili za mwaka 2020 zilizoandaliwa na kampuni ya Serengeti Byates maarufu kama Tanzania Digital Awards (TDA) 2020 baada ya kupata kura nyingi kutoka wadau mbalimbali na watumiaji wa huduma za Ki-uhamiaji na kushindanishwa na taasisi mbalimbali katika vipengele vya Digital Innovation of the year na Best Government Agency on Digital ambapo Uhamiaji ilishinda tuzo zote hizo.
Akipokea tuzo hizo katika ofisi za Uhamiaji Kurasini Dar es salaam Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala ameishukuru kampuni hiyo kwa kuandaa mashindano hayo kwani yamesaidia kujua namna gani huduma za ki-uhamiaji zinawafikia watanzania na raia wa kigeni kwa viwango bora vya kitaifa na kimataifa.
Aidha Dkt. Makakala amewashukuru wale wote walioshiriki kuipigia kura Idara ya uhamiaji katika vipengele vyote na hatimae kupata ushindi huo mkubwa ambao unabaki kuwa alama kubwa na kuwaahidi kuongeza uhodari na weledi wa hali ya juu ili kuongeza ufanisi zaidi katika kutoa huduma za Ki- Uhamiaji kwa faida ya kizazi cha sasa na baaae
Akikabidhi tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Byates Kennedy Mmali amepongeza Idara ya Uhamiaji kwa Ushindi huo kwani wamekuwa wabunifu zaidi kiasi cha kuzishinda taasisi nyingine za serikali.
Mashindano hayo ya Serengeti Byates kwa mwaka 2020 yalihusisha taasisi zaidi ya 50 za serikali na hatimaye uhamiaji kuibuka kidedea.
Hafla hiyo ya kukabidhi tuzo pia ilihudhuliwa na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Pasipoti na Uraia (CI) Gerald Kihinga, Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Udhibiti wa Mipaka (CI) Samweli Mahirane, Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Vibali vya Ukaazi Visa na Pasi (CI) Mary Palmer ndc na Pasi pamoja na Maafisa na Askari wa Uhamiaji.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akipokea tuzo za Tanzania Digital Awards 2020 kutoa kwa waandaaji kampuni ya Serengeti Byates |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni