Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

17 Aprili 2021

Uhamiaji Zanzibar Yachangia Damu Kwa Hiari

Zanzibar

Idara ya Uhamiaji Zanzibar mapema wiki hii imefanya zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari kwa Maafisa, Askari na watumishi raia wa Idara ya Uhamiaji wanaofanya kazi Zanzibar, zoezi ambalo limefanyika Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar.

Kaimu Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar DCI Nassra Juma Mohamed amewakaribisha waratibu kutoka Wizara ya Afya kitengo cha damu salama na kuwaahidi ushirikiano mzuri katika kufanikisha zoezi hili.

DCI Nassra amewashajihisha watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuchangia damu na kueleza kwa ufupi umuhimu wa suala la uchangiaji wa damu kwa watumishi.

Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya kuchangia damu Zanzibar Bwana Bakari Hamad Magarawa, amefafanua kuwa zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari ni kawaida kufanyika katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuhamasisha watumishi kujitokeza kuchangia damu kwa wingi, kwani hakuna tatizo la kiafya linalotokana na kuchangia damu.

Aidha amewaomba watumishi kuanzisha klabu ya uchangiaji damu “donor club” itakayosaidia mtumishi yoyote kufaidika endapo atapata tatizo la upungufu wa damu.

Bwana Magarawa ameendelea kueleza faida nyengine ya uchangiaji wa damu kwa watumishi ikiwa ni pamoja na mtu kupewa kadi ya uanachama ya kuchangia damu ambayo itamsaidia yeye na familia iwapo itapata tatizo la upungufu wa damu.

Jumla ya watumishi 35 wamejitokeza katika zoezi hilo la uchangiaji damu salama na kufanya zoezi la uchangiaji damu salama kufanikiwa katika kiwango kizuri.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kaimu Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar DCI Nassra Juma Mohamed akiwakaribisha waratibu kutoka Wizara ya Afya kitengo cha damu salama na kuwaahidi ushirikiano mzuri katika kufanikisha zoezi hilo





Zoezi la Uchangiaji Damu likiendelea







(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Zanzibar)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni