Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

07 Desemba 2020

Chuo cha Uhamiaji TRITA-Moshi Chaendelea kuwapika Washiriki wa mafunzo ya Masuala ya Ki-uhamiaji

Moshi, Kilimanjaro

Chuo cha Uhamiaji TRITA, Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kimendelea kuwapika Washiriki wa Mafunzo ya Masuala ya Ki-Uhamiaji kutoka katika taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi.

Akifungua Mafunzo hayo ya siku tano Mwakilishi wa Kaimu Mkuu wa Chuo TRITA-Moshi Naibu Kamishna Abdalah Towo, Kaimu Mkufunzi Mkuu wa Chuo hicho, Mrakibu Ignitious Mgana aliwapongeza washiriki wliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo muhimu sana kwao na Taifa kwa ujumla.

“Nitumie fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa ya kuteua Mawaziri na Manaibu Waziri ambao kwa kwa pamoja watakwenda kutekeleza kwa ufasaha na ueledi mkubwa falsafa yake ya “HAPA KAZI TU” na kuliletea taifa letu maendeleo zaidi” alisema Mrakibu Mgana.

Aidha amempongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt, Anna Peter Makakala ambaye kwa juhudi zake binafsi amekuwa akihakikisha kwamba mafunzo haya yanafanyika na amekuwa akifuatilia kwa karibu sana maendeleo ya mafunzo hayo.

Mrakibu Mgana amewakumbusha wasjiriki kwamba, mafunzo yao yameandaliwa mahususi kabisa ili kuwawezesha kuyafahamu masuala ya Ki-uhamiaji na Idara ya kazi, huku yakilenga katika kuimarisha uhusiano na kuboresha utoaji wa huduma kwa Watanzania na wageni waishio na kufanya kazi hapa nchini.

Mafunzo haya nia  ya Kundi la Kumi (OPARESHENI UHURU), yamekuja kufuatia uwelewa mdogo wa wadau mbalimbali kuhusu sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayotawala huduma za Uhamiaji na Idara ya Kazi, Suala hilo limekuwa likisababisha taasisi nyingi kujikuta zinaangukia mikononi mwa vishoka na matapeli.

Kupitia Mafunzo hayo washiriki watajifunza mambo mengi kuhusu  vibali vya Kazi na Ukaazi, uraia,visa, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka sanjari na masuala mengine kadha wa kadha.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kaimu Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji TRITA-Moshi, Mrakibu Ignitious Mgana akitoa hotuba kwa washiriki wa mafunzo
Picha ya Pamoja na Washiriki
Afisa Uhamiaji Wilaya ya Mwanga na Mkufunzi wa Chuo cha Uhamiaji TRITA Mrakibu Lydia Moshi
Akitoa neno kwa washiriki wa Mafunzo

Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Chuo cha Uhamiaji TRITA Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Leslie Mbota akitoa neno kwa washiriki (hawapo pichani)

Mkaguzi Msaidizi  Doroth Ngai akifundisha washiriki wa mafunzo ya masuala ya Ki-Uhamiaji ( hawapo pichani)Washiriki
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano chuo cha Uhamiaji TRITA- Moshi)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni