Zanzibar
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar (CI) Johar M. Sururu mapema wiki hii amezindua Jengo la Afisi ya Uhamiaji iliyoko Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kampuni ya Albatna Building Contractors co. LTD kukamilisha Ukarabati wake.
Akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia wakati
wa makabidhiano hayo Kamishna Sururu ametoa maelekezo ya kuhakikisha Majengo
hayo yanatunzwa, yanathaminiwa na yanawekewa mazingira mazuri kwa manufaa ya
Kizazi cha sasa na baadae.
Aidha amesisitiza kuzingatia umuhimu wa upatikanaji
wa majengo mapya uende sambamba na utoaji wa huduma bora zenye kiwango cha
kitaifa na Kimataifa sanjari na kuwataka kufanya kazi kwa Utii, Uhodari na
Weledi wa hali ya juu.
“Tunataka huduma zetu ziendane na Jengo hili jipya
na sitarajii kusikia malalamiko kutoka kwa wananchi “Alisema
Kwa upande wake Mhandisi wa Kampuni Albatna
Building Contractors Co. ltd Bwana Seif M. Said alisema, ukarabati huo
umefanyika kwa kuzingatia muda ulioweka pamoja na vigezo vyote villivyohitajika
ili jengo liweze kudumu kwa muda mrefu.
Idara ya Uhamiaji Tanzania imeendelea kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya Idara na Taifa kwa ujumla, hali
inayopelekea kuimarisha haiba ya usalama wa majengo na kukuza uchumi wa Taifa.
Makabidhiano |
![]() |
Muonekano wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya Kukarabatiwa (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Zanzibar) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni