Dodoma
Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala mapema wiki hii amefanya ziara katika eneo la
Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma na Kutoa
Maelekezo kwa Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT Kuongeza kasi ya Ujenzi ili kumaliza
Jengo hilo mapema iwezekanavyo.
CGI Dkt. Makakala
amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kufanya kazi Usiku na Mchana ili jengo hilo
liweze kukamilika kwa haraka.
Hata hivyo Dkt.
Makakala ametoa pongezi kwa Mkandarasi huyo kwa kujenga jengo lenye ubora litakalochangia katika kuboresha huduma bora za Ki-Uhamiaji zinazokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.
Jengo hilo lenye ghorofa 08 litakapokamilika linaweza kuwa la kwanza kwa Ukubwa hapa Jijini Dodoma.
HABARI PICHA NA MATUKIO
 |
Muonekano wa Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo Jipya la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu ya Nchi Dodoma |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akisaini Kitabu cha wageni |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akiangalia Ubora wa baadhi ya milango itakayotumika katika eneo la Basement |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akiendelea na Ukaguzi |
 |
Mafundi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT Wakiendelea na kazi ya kumwaga nzege katika Jengo Jipya la Makao Makuu ya Uhamiaji Jijini Dodoma |
 |
Kazi Inaendelea |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akiangalia baadhi ya vifaa vinavyotumika kufanyia kazi. |
 |
Kazi ya Nzege ikiendelea |
 |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni