Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

11 Desemba 2020

DCI Towo Awataka Wahitimu wa Mafunzo ya Masuala ya Ki-Uhamiaji Kutojihusisha na Rushwa.

Moshi, Kilimanjaro

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Ramadhan Towo amewataka washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa masuala ya Ki-Uhamiaji kwa taasisi za Umma na Sekta Binafsi kutojihusiha na Rushwa.

Ameyasema hayo mapema leo katika hafla ya kufunga mafunzo hayo ya siku 05 kwa washiriki kutoka katika taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi Kundi la 10 (Oparesheni Uhuru) ambapo amewataka kuwa waadilifu na kamwe wasijaribu kutoa wala kupokea Rushwa .

“Ndugu Wahitimu; mara nyingi sana Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekuwa anakemea vitendo vya Rushwa, hivi karibuni alipokuwa akiwaapisha Mawaziri na Manaibu mawaziri, alilisitiza uadilifu na pia alikemea vitendo vya Rushwa” Alisema DCI Towo.

Kaimu Mkuu huyo wa Chuo DCI Towo aliwakumbusha wahitimu kwamba, rushwa ni tatizo kubwa linalozorotesha ustawi wa jamii duniani kote, aidha, kwa upande wa Afrika na nchi zinazoendelea tatizo la rushwa limeonekana kuleta athari zaidi katika ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Hivyo ameisitiza kwamba Mafunzo waliyoyapata chuoni TRITA yakawasaidie kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa wazalendo kwa kumsaidia Mhe. Rais Magufuli katika juhudi zake za kuipandisha nchi yetu kiuchumi na katika mikakati yake ya maendeleo pamoja na kuhakikisha kwamba miradi yote inafanikiwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Kwa upande mwingine, DCI Towo Kwa niaba ya Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala, ameushukuru Uongozi wa HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO - KINAPA kwa kuendelea kushirikiana na Chuo kwani wamekuwa wakitoa fursa ya mara kwa mara kupeleka washiriki katika hifadhi hiyo lakini pia mara zote wamekuwa wakiandaa darasa maalum kwa washiriki kujifunza na hivyo, ameomba uhusiano huo uzidi kuleta chachu ya maendeleo kwa taasisi za umma na binafsi na kwa maslahi mapana ya taifa.

“Nampongeza sana Ndugu Paul Kayanda kwa maneno yake ya busara aliyoyatoa alipokuwa anatoa neno la shukurani kwa niaba yenu, nimefarijika sana kuona kwamba nanyi mmeona umuhimu wa mafunzo ya namna hii, msisahau kuwaeleza wengine juu ya mafunzo haya, na natumaini mtatusaidia sana kupata mawasiliano yao ili nao tuweze kuwatumia mwaliko” Alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wahitimu Bw. Paul Kayanda ammepongeza na Kumshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala kwa Kuanzisha Programu hiyo ya Mafunzo ya usimamizi wa masuala ya Ki-Uhamiaji kwa taasisi za Umma na Sekta Binafsi kwani ni msaada mkubwa sana kwao katika kurahisha utendaji wa kazi zao sanjari na kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Taifa.

Mafunzo haya ambayo bado yanaendelea kuendeshwa kila mwezi, hivi sasa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda – TRITA kinaandaa mafunzo mengine maalum ambayo yatawakutanisha washiriki wa makundi yote kumi ambayo tayari yamepata mafunzo ya namna hii, mipango na taratibu zingine zikikamilika basi mwaliko utatumwa kwa washiriki wote.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), Moshi Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo akiwa katika Picha ya Pamoja Wahitimu wa mafunzo Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Moshi Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Ramadhan Towo akiongea na Vyombo vya Habari


Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Mrakibu Leslie Mbotta akiongoza itifaki katika hafla ya kufunga Mafunzo ya Masuala ya Ki-Uhamiaji

Washiriki wakipokea vyeti

Bw. Paul Kayanda akitoa Shukrani kwa niaba ya Wahitimu

Mhifadhi Idara ya Utalii KINAPA Herman Mtei  Akitoa Historia ya Mlima Kilimanjaro kwa Washiriki wa Masuala ya Ki-Uhamiaji
Mhifadhi Idara ya Utalii KINAPA  Herman Mtei Akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa Washiriki wa Masuala ya Ki-Uhamiaji

(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni