Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, mapema wiki hii amefanya ziara katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma na Kutoa Maelekezo kwa Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT Kufanya kazi masaa 24.
Mhe. Simbachawene amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ya Ujenzi kwa kufanya kazi Usiku na Mchana ili jengo hilo liweze kukamilika kwa haraka.
Amesema jengo hilo la ghorofa nane lilipaswa kukamilika mwezi Disemba, 2020, lakini mpaka sasa lipo asilimia 41 jambo ambalo hajaridhishwa nalo.
Hata hivyo Mhe. Simbachawene alitoa pongezi kwa Mkandarasi huyo kwa kujenga jengo lenye ubora mkubwa litakalochangia katika kuboresha huduma bora za Ki-Uhamiaji zinazokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.
"Jengo hili litakapokamilika linaweza kuwa la kwanza hapa Dodoma kwa ukubwa, hivyo nawataka Wajenzi hawa kuongeza kasi ili tuweze kuhamia hapa mapema iwezekanavyo," alisema Mhe. Simbachawene.
Idara ya Uhamiaji Inaendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwemo Kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo ili kulinda Usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya Kichumi huku ikiongozwa na Kauli mbiu ya Uhamiaji, “Usalama na Maendeleo”
MATUKIO KATIKA PICHA
![]() |
Muonekano wa Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Tanzania linaloendelea kujengwa Jijini Dodoma |
![]() |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Konstebo wa Uhamiaji Innocent Swallo Kutoka Kitengo cha Majengo Uhamiaji Makao Makuu |
![]() |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni |
![]() |
Ukaguzi Ukiendelea |
![]() |
Ujenzi Ukiendelea |
![]() |
Ukaguzi Ukiendelea |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni