Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

06 Desemba 2020

Uhamiaji Tanzania yapongezwa kwa Utendaji Kazi Bora Uliotukuka.

Moshi, Kilimanjaro

Idara ya Uhamiaji Tanzania Imepongezwa kwa utendaji kazi Uliotukuka na unaotoa huduma bora za Kiuhamiaji zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Bw. Ramadhan Kailima, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi  TUGHE Tawi la Uhamiaji lililofanyika katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili na kufanya tathimini ya utekelezaji wa majukumu ya Idara, katika kipindi cha Robo ya Kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021.

“Nichukue fursa hii kuipongeza Idara ya Uhamiaji kwa kutekeleza wajibu na majukumu yenu kwa ufanisi, weledi na uhodari wa hali ya juu, kwani kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2020 mmefanikiwa kukamata jumla ya wahamiaji haramu 15,600 ambapo kati yao 10,500 mmewarejesha nchi walizotoka, 2,000 wamefungwa gerezani na waliobaki mnaendelea na Mashauri yao  Mahakamani” Alisema

Aidha Idara imefanikiwa pia kuwakamata Watanzania 45 ambao  ni Vinara wa Usafirishaji wahamiaji haramu ambao tayari wamefikishwa mahakamani na sheria imechukua mkondo wake.

Bw. Kailima alibainisha pia kuhusu mafanikio ya uhamiaji katika kuongeza urahisi wa utoaji wa Vibali  kwa haraka na Visa  na kuondoa uwezekano wa kughushi vibali.

Idara kwa kipindi cha Februari  2019 hadi Disemba 2020 imefanikiwa kuongeza utoaji wa vibali vya ukaazi ambapo vibali vya ukaazi daraja “A”  1,649 na kufanikiwa kukusanya Usd 4,792.

Vibali vya Ukaazi daraja “B” Vilitolewa 6,902 na kufanikiwa kukusanya  Usd 14,321 na daraja “C” vilitolewa vibali 4,126 na kufanikiwa kukusanya Usd 13,112.

Naibu Katibu Mkuu Bw. Kailima alienda mbali zaidi na kubainisha kwamba Idara ya Uhamiaji pia imeboresha na kuimarisha mfumo wa utoaji wa Visa za Kielekroniki ambao umesaidia kukusanya maduhuli ya serikali ambapo jumla ya dola za Kimarekani  22, 112,001 zilikusanywa kwa kipindi cha Julai 2019 mpaka Novemba 2020, sanjari na kasi ya ongezeko la utoaji wa Pasipoti za Kielekroniki zenye ubora na usalama wa hali ya juu.   

Kwa Upande wake Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala alisema Idara ya Uhamiaji ni miongoni mwa Taasisi za kijeshi hapa nchini, ambayo Inawatumishi Maofisa, Askari na Raia.

Watumishi hao wamekuwa wakishirikiana vyema katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Idara ya Uhamiaji kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo, na kwa kuzingatia umuhimu wa kila Kada katika utekelezaji wa majukumu husika.

Aidha, Idara imekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano inayohusisha watumishi wa Kada zote mahala pa Kazi ili kujadili na kusikiliza hoja zao pamoja na kutoa miongozo mbalimbali ya utendaji.

“Napenda kukutaarifu kuwa, kwa sasa tunao uhusiano thabiti kati ya Menejimenti ya Idara ya Uhamiaji na Tawi la TUGHE Uhamiaji, Kwa sasa Watumishi raia wanatumia chombo hiki kufikisha hoja walizo nazo kwa Uongozi wa Idara kwa njia muafaka, Ninachoweza kusema hapa Ndugu Mgeni Rasmi ni kwamba, Uongozi wa Idara ya Uhamiaji utaendelea kudumisha upendo miongoni mwa watumishi wote pasipo ubaguzi wa kada yoyote” Alisema CGI Dkt. Makakala.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima Katikati Akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wakuu wa TUGHE Tawi la Uhamiaji

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Wafanyakazi wa TUGHE Tawi la Uhamiaji
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa TUGHE na Makamishna wa Uhamiaji Tanzania Waliosimama Nyuma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa TUGHE Tawi la Uhamiaji


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Maafisa Uhamiaji Mikoa Kulia Kwake ni Kamishna wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala na wa Kwanza Kulia waliokaa ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar (CI) Johar Sururu

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wakuu wa Vitengo kutoka Idara ya Uhamiaji Tanzania



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa TUGHE Tawi la Uhamiaji













Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania CGI Dkt. Anna Makakala




Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Katikati) Akiteta jambo na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Samwel Mahirane (Mwenye koti la Bluu) na Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro ACI Martin Mwenda

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Nchini Mrakibu Paul Mselle, wa Kwanza (Kushoto), Kulia ni Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Chuo cha Uhamiaji RITA-Moshi Mrakibu Msaidizi  Leslie Mbota na Katikati ni Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini Bw. Felix Mwagala Kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Wakibadilishana Mawazo Wakati wa kutano wa TUGHE Tawi la Uhamiaji 


Kamishna wa Uhamiaji Uraia na Pasipoti (CI) Gerald Kihinga

Kamishna wa  Uhamiaji Utawala na Fedha (CI) Edward Chogero


(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni