Zanzibar
Timu ya mpira wa miguu ya Uhamiaji Zanzibar mapema wiki hii imeanza vyema katika mechi zinazoendelea kuchezwa Visiwani humo, ikiwa ni mechi za ligi daraja la kwanza kanda ya Unguja.
Timu hiyo imeibuka kidedea kwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya mpinzani wake Mchangani United iliyojinyakulia bao moja katika dakika ya 56 katika mechi iliyochezwa katika viwanja vya Mau.
Mabao hayo kwa upande wa Uhamiaji FC yamefungwa na mchezaji Kassim Ramadhan katika dakika ya 12 na Haji Khamis Mnachia katika dakika ya 46 na kupelekea ushindi huo.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kikosi cha Timu ya Uhamiaji Zanzibar |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Afisi Kuu Zanzibar) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni