Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

10 Desemba 2020

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Aipongeza Uhamiaji kwa Kuendelea Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Nchi Mipakani.

 Moshi, Kilimanjaro

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima amewataka Maofisa Askari na Watumishi kutoka taasisi mbalimbali zinazofanya kazi katika kituo cha pamoja cha Forodha Mpakani, Holili OSBP kuhakikisha wanakusanya maduhuli ya serikali kwa manufaa ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kituo hicho cha pamoja cha forodha Holili OSBP kilichopo Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro, sanjari na kukagua vipenyo mbalimbali vinavyotumika kupitishia Wahamiaji haramu wanaoingia nchini Kinyume cha utaratibu na sheria. 

Katika kuendelea kuimarisha masuala ya Ulinzi na Usalama mpakani Naibu Katibu ameipongeza Idara ya Uhamiaji nchini kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama hasa wakati wa uingiaji na utoakaji wa wageni na raia wa Tanzania katika maeneo ya Mipaka kote nchini sanjari na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama wa Taifa.

Pamoja na Pongezi hizo ameitaka Idara ya Uhamiaji kuongeza juhudi zaidi katika kufanya doria na misako ya mara kwa mara katika vipenyo mbalimbali vya wahamiaji haramu ili kukomesha kabisa wimbi la wahamiaji haramu ambalo ni hatari kwa usalama wa Taifa.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi ya kituo hicho Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Holili OSBP Mrakibu Michael Mtoba alisema  katika kuimarisha ulinzi na usalama wa mpaka wamekuwa wakishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama sanjari na taasisi nyingine za serikali zinazofanya kazi mpakani.

“Hali ya mpaka wetu wa Holili ni shwari, shughuli za uvushaji mizigo kwa kutumia malori ya mizigo zinaendelea vema na hakuna hali ya uvunjifu wa amani,tishio au tendo lolote  linaloleta taharuki kwa kituo au serikali kwa ujumla” alisema Mrakibu Mtoba.

Kituo cha pamoja cha Forodha Holili  ni mpaka ulioanzishwa kwa sheria ya EAC-One stop Border post  ya mwaka 2016 ambapo watu pamoja na vyobo vya moto vinavyovuka mpaka husimama mara moja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za utokaji na uingiaji nchini, kwa  misingi hii katika OSBP taratibu za kutoka na kuingia nchini zinafanyika  mahala pamoja paitwapo Common Contro Zone, huku lengo kuu la uanzishwaji wake likiwa ni kuwezesha biashara kupitia mipaka (Cross Border trade) kwa kupunguza muda unaotumika kutoa huduma mipakani.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima akipokelewa na Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Holili OSBP Mrakibu Michael Mtoba wakati wa ziara yake ya kikazi hivi karibuni



Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka CI Samwel Mahirane nae akisalimiana na baadhi ya watumishi wa taasisi  mbalimbali za serikali zinazofanya  kazi Holili OSBP


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima akipokea maelezo mafupi kutoka kwa Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Holili OSBP Mrakibu Michael Mtoba wakati wa ziara yake ya kikazi hivi karibuni


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kulia) akipokea maelezo mafupi ya Ramani ya Mpaka wa nchi kutoka kwa Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Holili OSBP Mrakibu Michael Mtoba wakati wa ziara yake ya kikazi hivi karibuni Kushoto Pichani ni Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka CI Samwel Mahirane


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kulia) akipokea maelezo mafupi ya Jiwe la Mpaka (Kati ya Kenya na Tanzania)  






Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kulia) akipokea maelezo mafupi ya namna (TRA) Inavyofanya kazi zake katika kituo hicho cha Holili OSBP



Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka CI Samwel Mahirane akieleza jambo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima akisaini kitabu cha wageni

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro ACI Edward Mwenda akisaini Kitabu cha wageni katika kituo cha Uhamiaji Holili OSBP

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kushoto) akipokea maelezo mafupi ya namna Shirika la Viwango TBS linavyotekeleza Majukumu yake mpakani hapo


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kulia) akipokea maelezo mafupi ya Ukaguzi wa Mizigo



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kulia) akipokea maelezo mafupi ya vipenyo  vinavyotumika na wahamiji haramu kuingia nchini kinyume cha sheria


Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka CI Samwel Mahirane akieleza namna Iara ya Uhamiaji ilivyojipanga Kupambana na Wahamiaji Haramu





Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Kulia) akioneshwa vipenyo  vinavyotumika na wahamiji haramu kuingia nchini kinyume cha sheria (kushoto) ni
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka CI Samwel Mahirane


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima (Katikati) akioneshwa mpaka wa Tanzania na Kenya  




(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni