Na. Mwandishi wetu Dodoma, Tanzania
Jeshi la Uhamiaji Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita lilipokea ujumbe wa Wakufunzi 30, na Wanafunzi 43 wa Mataifa mbalimbali, kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kwa ajili ya ziara ya kupatiwa mafunzo ya namna Jeshi la Uhamiaji linavyofanya shughuli zake katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.
Ziara hiyo ya mafunzo ilifanyika katika Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Jijini Dodoma huku ikiongozwa na Brigedia Jenerali Chelestino Msola na kupokelewa na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga ambae alimwakilisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.
Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali ziliwasilishwa na Maafisa kutoka Jeshi la Uhamiaji hususani Pasipoti, Visa za Kielektroniki, Uraia pamoja na mifumo inayotumika katika utoaji wa Pasipoti na visa za kieletroniki.
Aidha, Washiriki wa ziara hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa ipasavyo sanjari na Kutembelea maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma.
Kwa upande wao washiriki walimpongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kwa mafunzo waliyoyapata na kuongeza kuwa, mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu hususani katika kuwahudumia wananchi.
Baada ya kuhitimisha ziara ya mafunzo kwa wanafunzi wa chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) katika Makao Makuu ya Jeshi la Uhamiaji Jijini Dodoma ziara hiyo iliendelea tena katika vyombo vingine vya ulinzi na usalama hapa nchini.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga akiongea na baadhi viongozi wa ujumbe kutoka chuo cha Taifa cha Ulinzi wa Taifa (NDC) walipofika Uhamiaji makao makuu kwa ajili ya ziara ya mafunzo |
|
Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC Wakiwa tayari kupatiwa shule ya masuala ya kiuhamiaji |
|
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle akiratibu mafunzo ya masuala ya Uhamiaji wakati wanafunzi kutoka chuo cha ulinzi wa Taifa NDC walipofika kwa ajili ya kujifunza |
|
Mrakibu wa Uhamiaji Azizi Kilondomara akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa NDC |
|
Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola Akieleza lengo la ziara yao katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu Dodoma |
|
Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi Jarida la NDC Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga |
|
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga (Kulia) Aakimkabidhi Kalenda ya Uhamiaji Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola |
|
Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya mwavuli wenye nembo ya NDC Mrakibu wa Uhamiaji Eliud Ikomba ambaye aliwasilisha mada moja wapo ya masuala ya Uhamiaji kwa wanafunzi wa NDC |
|
Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya kofia yenye nembo ya NDC Mrakibu wa Uhamiaji Azizi Kilondomara ambaye nae aliwasilisha mada moja wapo ya masuala ya Uhamiaji kwa wanafunzi wa NDC |
|
Mkuu wa Msafara wa Wanafunzi kutoka NDC Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kofia yenye nembo ya NDC Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle |
|
Ziara katika Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma |
|
Muonekano wa maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma |
|
Mtaalamu wa Ujenzi kutoka SUMAJKT akitoa maelezo ya ujenzi |
|
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ulinzi wa Taifa NDC wakifurahia jambo |
|
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni