Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

12 Oktoba 2020

Chuo cha Uhamiaji chaendelea kutoa Mafunzo ya Masuala ya Kiuhamiaji kwa Taasisi na Sekta Binafsi

Moshi, Kilimanjaro
Idara ya Uhamiaji kupitia chuo chake Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kimeendelea kutoa mafunzo kwa Taasisi za Umma na Sekta binafsi ili kuwajengea uwezo juu ya masuala ya Uhamiaji 

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo siku ya Ijumaa, Kaimu Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo amesema  lengo la kuwapa mafunzo ni kuwajengea uwezo wa kuzifahamu Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia masuala ya Uhamiaji hapa nchini.

Aidha mafunzo hayo kwa ujumla yalilenga pia katika kuwajengea uelewa na maarifa washiriki  ili kuwawezesha kuwa na weledi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi. 

"Wengi wenu ni Maafisa Utumishi katika Taasisi au Makampuni ambapo mnaajiri wageni, hivyo ni wajibu wetu kuwaelimisha taratibu mbalimbali ili wageni wenu waishi na kufanya kazi nchini pasipo kuvunja sheria za Uhamiaji." Alisema Towo.

Hata hivyo DCI Towo aliendelea kueleza kwamba katika masomo yao washiriki walikuwa wakijadidili hoja mbalimbali  na baadhi tayari zimechukuliwa na zinaingia katika Taarifa ya  kuwasilisha kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala kwa ajili ya maamuzi ambapo utekelezaji wake utafuata na utaleta manufaa mengi kwenye Idara na Nchi kwa Ujumla.

Nae mmoja wa wahitimu kutoka Kampuni ya Fluiconecto Tanzania Ltd ya mjini Mwanza Bi. Azza Hilal alisema mafunzo haya yamemuwezesha kujua taratibu zinazotakiwa kufuata ili kumuajiri raia wa kigeni katika kampuni yake.

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza Oktoba 5 na kumalizika Ijumaa Oktoba 9 huku yakishirikisha Washiriki 30 ambao wamehitimu na kupatiwa vyeti vya ushiriki.

Washiriki hao Walipata pia fursa ya Kutembelea Hifadhi ya  Mlima Kilmanjaro (KINAPA) na baadae kutoa zawadi ya Keki kwa Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo

Kwa Ujumla Mafunzo haya ni mwendelezo wa Programu za  Idara ya Uhamiaji kupitia chuo chake cha TRITA katika kuwaelimisha wadau wanaohusika na raia wa kigeni hapa nchini sanjari na kutoa huduma za Ki-Uhamiaji zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa na hatimae kulinda Usalama wa Taifa ili Kukuza Maendeleo ya Kiuchumi kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Kaimu Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo Akitoa Cheti kwa mmoja wa Washiriki wa Mafunzo


Washiriki wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Kaimu Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo (Hayupo Pichani)

Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Chuo cha Uhamiaji TRITA-Moshi Mrakibu Msaidizi (ASI)Leslie Mbotta Akiwashukuru Washiriki kwa kuonesha ushirikiano wa kutosha wakati wa Mafunzo yaoWashiriki wa Mafunzo ya Ki-Uhamiaji TRITA wakiwa katika Picha ya Pamoja (katikati) ni Mkuu wa Chuo cha TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Towo (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni