Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amempongeza Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Mzee Mkongea Ali kwa kuiwakilisha vyema Idara ya Uhamiaji
katika Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2019.
“Nakupongeza
sana kwa kazi nzuri uliofanya katika Taifa letu. Nimefurahi sana kwa uwakilishi
wako uliotukuka, kwa kweli umeibeba vyema bendera ya Uhamiaji, unastahili pongezi
za dhati, pamoja na kwamba uko likizo lakini nimeona nikuite uje nikupongeze”
Alisema Dkt. Makalala
Kwa upande
wake Mkaguzi Msaidizi Mzee Mkongea alimshukuru Kamishna Jenerali, Makamishna na
Viongozi waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kwa Miongozo, Ushauri na Maelekezo yao
ya mara kwa mara yaliyomuwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wote
wa mbio hizo.
Mzee Mkongea
Ali ambaye ni Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mjini Magharibi alikuwa Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019 ambapo ameifanya kazi hiyo kwa bidii,
uadilifu, utiifu na uzalendo hadi kufikia kilele cha mbio hizo na kuzimwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
mjini Lindi tarehe 14 Oktoba 2019.
Unaitwa "MWENGE WA UHURU" sio "Mwenge", hivyo ni "mbio za Mwenge wa Uhuru" na sio "mbio za Mwenge"
JibuFuta