Matangazo

📢 IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA — KARIBU KWENYE BLOG RASMI   ✦   📰 UHAMIAJI HABARI BLOGU — TUNAKULETEA MATUKIO KILA SIKU   ✦   📲 FUATA IDARA YETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII   ✦   ✉️ WASILIANA NASI: info@immigration.go.tz   ✦   ☎️ +255-22-2850575/6

25 Oktoba 2019

Dkt. MAKAKALA AMPONGEZA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2019









Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amempongeza Mkaguzi  Msaidizi wa Uhamiaji Mzee Mkongea Ali  kwa kuiwakilisha vyema Idara ya Uhamiaji katika Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2019.

“Nakupongeza sana kwa kazi nzuri uliofanya katika Taifa letu. Nimefurahi sana kwa uwakilishi wako uliotukuka, kwa kweli umeibeba vyema bendera ya Uhamiaji, unastahili pongezi za dhati, pamoja na kwamba uko likizo lakini nimeona nikuite uje nikupongeze” Alisema Dkt. Makalala

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi Mzee Mkongea alimshukuru Kamishna Jenerali, Makamishna na Viongozi waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kwa Miongozo, Ushauri na Maelekezo yao ya mara kwa mara yaliyomuwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wote wa mbio hizo.

Mzee Mkongea Ali ambaye ni Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mjini Magharibi alikuwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019 ambapo ameifanya kazi hiyo kwa bidii, uadilifu, utiifu na uzalendo hadi kufikia kilele cha mbio hizo na kuzimwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mjini Lindi tarehe 14 Oktoba 2019.

Maoni 1 :

  1. Unaitwa "MWENGE WA UHURU" sio "Mwenge", hivyo ni "mbio za Mwenge wa Uhuru" na sio "mbio za Mwenge"

    JibuFuta