Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi hizo wakati alipokuwa na mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Peter Makakala, aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar, kwa ajili ya kujitambulisha.Katika maelezo
yake, Rais Dkt
. Mwinyi alitoa pongezi kwa Idara hiyo ya Uhamiaji kwa kuanza
kuzifanyia kazi changamoto zilizokuwepo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani karume hatua ambayo itapunguza foleni kwa wasafiri wakiwemo wageni
ambao lengo ni warudi tena kuja kuitembelea Zanzibar.
Alisema kuwa
changamoto ya foleni ilikuwa ikiwasumbua sana wasafiri wakiwemo wageni hasa
ikizingatiwa kwamba uwanja wa ndege huo ni lango la watalii kutoka nje ya nchi
hivyo, kupatikana na ufumbuzi huo kutaweza kusaidia.
Aliongeza kuwa
juhudi za makusudi zitachukuliwa katika kuhakikisha jengo jipya la uwanja wa
ndege litakapoanza kazi changamoto kama hizo hazijitokezi.
Alipongeza kwa
kuongeza kwa madawati na kufikia 28 ambazo zimeanza kusaidia na kupunguza foleni
katika uwanja wa ndege huo hasa pale wakati zinazotua ndege nyingi kutoka nje
kwa wakati mmoja.
Sambamba na hayo,
Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Idara ya Uhamiaji
Zanzibar kwa kuzifanyia kazi changamoto hizo na kupelekea kuongeza madawati
katika uwanja huo wa ndege wa Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi alitoa ushauri kwa Idara hiyo ya Uhamiaji kuwa ni vyema kuhakikisha kila mgeni anaekuja awe ameshapata VISA yake ili kuondosha kukaa foleni muda mrefu katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Pamoja na hayo,
Rais Dk. Mwinyi alisisitiza kwamba kwa vile uchumi wa Zanzibar unaitegemea kwa
kiasi kikubwa sekta ya utalii hivyo, ni vyema kwa kila mdau kwa upande wake
akahakikisha anatoa mchango wake katika kufanikisha jambo hilo.
Rais Dk. Mwinyi
alitumia fursa hiyo kuipongeza Idara hiyo kwa kazi kubwa iliyoifanya ya
kushiriki katika kuleta amani nchini katika wakati wa uchaguzi hatua ambayo
bado wanaendelea nayo.
Aidha, alipokea
pongezi za kushinda nafasi ya kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba 2020.
Mapema Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala alimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa
kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliopoita wa Oktoba 2020 na kuwa Rais wa
Zanzibar Awamu ya Nane.
Dkt. Makakala alitoa
shukurani zake yeye pamoja na Idara yake ya Uhamiaji na kupongeza mashirikaino
yaliopo kati yake na Kamishna wa Uhamiaji wa Zanzibar Johari Masoud Sururu
hatua ambayo alisema inazidi kuiimarisha Idara hiyo.
Alisema kuwa kazi
za Idara hiyo zitaendelea kuimarishwa kwa weledi na kutoa ushirikiano sambamba
na kupokea maelezo kwa Rais Dkt. Mwinyi ili kuimarisha vyema kazi za Idara hiyo.
Alisema kuwa Idara
hiyo imeimarisha mifumo ya utoaji wa huduma na kuimarisha mfumo wa Uhamiaji
Mtandao ambapo tayari wameshaanza kutoa pasi za kusafiria za elektroniki ambapo
pasi hiyo iliweza kushinda kimataifa.
Aidha, alisema kuwa
Idara hiyo inatoa VIZA kwenye mitandao, vibali vya ukaazi pamoja na udhibiti wa
mipaka ambapo hatua hiyo imeweza kuimarisha mapato kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa tokea
mifumo hiyo ianze mapato yameweza kuongezeka ambapo mnamo mwaka 2015 kabla ya
kutumika kwa njia ya mifumo ya mtandao Idara hiyo ilikusanya Bilioni 10 kwa
upande wa Zanzibar na mwaka 2016 ilikusanya Bilioni 17.7 ambapo
mwaka 2017 ilikusanya Bilioni 23.
Aliendelea kueleza
kwamba kuanzia mwaka 2018 walipoanza kutumia mfumo mtandao Idara hiyo iliweza
kukusanya bilioni 28.9 na mwaka 2019 ilikusanya bilioni 31 ambapo mwaka 2020
ilikusanya bilioni 33 licha ya kuwepo changamoto kadha ikiwemo ugonjwa wa Covid
19.
Pamoja na
hayo,CGI Dkt. Makakala alisema kuwa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar
kumekuwa na changamoto ya kupambana katika kutoa huduma bora kwa watalii na
wananchi kutokana na ndege kutua kwa wakati mmoja sambamba na uwanja mmoja
kutumia ndege za ndani na nje.
Alisema
kuwa licha ya hali hiyo kutokana na kuimarisha mifumo wameweza
kuongeza madawati na kufikia 28 na kuweza kutoa huduma ambapo ndege yenye
abiria 400 wanaweza kuhudumia kwa saa moja.
Pia, kutokana na
uhaba wa wafanyakazi wa Idara hiyo imeweza kuongeza wafanyakazi kutoka 68 na
kufikia 113 huku wakichukua juhudi ya kuomba Mamlaka ya uwanja wa ndege kupeana
muda jambo ambalo limekubalika jambo ambalo litaleta faraja.
Kamishna Jenerali
huyo alieleza matarajio yake katika jengo jipya la uwanja wa ndege wa Abeid
Amani Karume (Terminal
III) linalotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni.
Alieleza juhudi
zilizochukuliwa kiwanjani hapo ambapo abiria hivi sasa hana haja ya kupita
katika sehemu nne za madawati kama ilivyokuwa hapo awali huku akieleza kwamba
tayari wameshapata vifaa ambapo wageni wanaweza kulipa hapo hapo uwanjani iwapo
watakuwa na kadi za benki.
Alisema kuwa mbali
ya kusimamia ulinzi na usalama Idara hiyo imehakikisha inachangia mapato na
uchumi wa nchi sambamba na kuendelea na kazi zake za kufanya misako mbali mbali
nchi nzima ili kuhakikisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila ya kufuata
taratibu wanachukuliwa hatua stahili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni