Maandamano hayo yalipokelewa na mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman.
Katika kufanikisha maadhimisho hayo michezo mbali mbali ilioneshwa ikiwa ni pamoja na mchezo wa kuvuta kamba na mazoezi mbali mbali kwa washiriki wote.
Walioshiriki uvutaji kamba ni majaji na wanasheria kutoka afisi ya Jaji Mkuu, afisi ya bandari, KMKM na kikundi cha kitambi noma ambapo washindi walitangazwa na kupongezwa na mgeni rasmi, Kmkm na kitambi noma ndio walikua washindi wa mchezo huo dhidi ya wanasheria na Bandari.
Aidha mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar aliwashukuru waandaaji wote pamoja na afisi ya Jaji mkuu kwa kufanikisha zoezi hilo, vile vile amewataka washiriki wote wawe na tabia ya kufanya mazoezi kila siku kitu ambacho kitawajengea afya imara.
Kuvuta Kamba |
Mazoezi yakiendelea |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Afisi kuu Zanzibar) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni