Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

10 Agosti 2020

Ziara ya CGI Dkt. Anna Makakala Wilayani Korogwe DC Kasongwa Atoa Kongole

Korogwe, Tanga

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala hivi karibuni amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga na kukutana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Kissa Gwakisa Kasongwa.

Akiongea na Kamati hiyo CGI Dkt. Makakala alisema lengo la ziara yake ya kikazi ni kuona namna Idara ya Uhamiaji ilivyojipanga katika kudhibiti wimbi la uingiaji wa  wahamiaji haramu nchini hasa katika wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.

“Nimetembelea Wilaya karibu zote za Mkoa wa Tanga  ili kuona namna  Idara yangu ya Uhamiaji ikiwa ni moja ya chombo cha Ulinzi na Usalama ilivyojipanga kuhakikisha kwamba ulinzi na usalama unaimarishwa  sanjari na kudhibiti uingiaji na utokaji wa wageni na raia  wa Tanzania  na kuhakikisha kwamba wahamiaji haramu hawatuvurugii uchaguzi wetu” alisema

Akitoa Maelekezo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapo CGI Dkt. Anna Makakala amevitaka vyombo hivyo vya ulinzi na  usalama kushirikiana kwa nguvu zote ili kuhakikisha ulinzi na usaslama unaendelea kuimarishwa nchini.

Aidha ametoa rai kwa kwa wananchi kote  nchini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wanapoona wageni wasiowatambua sanjari na wageni wote wote wanaoingia nchini kufuata sheria na taratibu za nchi yetu kwa manufaa ya ulinzi na usalama wa Taifa letu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Korogwe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa akitoa taaarifa ya hali ya ulinzi na usalama ya wilaya alisema Wilaya iko shwari, hali ya ulinzi na usalama inaridhisha na  wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Na tumekuwa tukikuona kwenye TV sisi tumefurahi sana kukuona Live na ukiwa ni mmoja wa wanawake ambao ni wapambanaji na wanaotazamwa sana wewe ni (Role model) wetu katika nchi yetu hii ya Tanzania, hii ni kutokana na uongozi wako imara na uliotukuka, kwani unaliongoza vyema Jeshi la Uhamiaji  kwa Uhodari na weledi wa hali ya juu hongera sana  kwa majukumu ya kazi  mama yetu” alisema DC Kasongwa

DC Kasongwa aliongeza kwamba katika Wilaya ya Korogwe kwenye upande wa Uhamiaji  wamepata Afisa Uhamiaji mpya (W) anaefanya kazi vizuri sana  na anatoa ushirikiano na wenzake katika kamati ya Ulinzi na Usalama, kwa kipindi chake zaidi ya wahamiaji haramu 60 waliweza kukamatwa na kufikishwa mahakamani na wengine kurudishwa kwao.

Ziara ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini ni muendelezo wa ziara zake za kikazi ambapo huzifanya mara kwa mara kwa lengo la kukagua hali ya mipaka ya nchi, na kukagua utendaji kazi wa Maofisa  na askari katika maeneo yao ya kufanyia kazi.  

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala (Kushoto) Akipokelewa na Mkuu wa Wilaya Korogwe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala (Kushoto)akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe (DAS) Bi. Rahel Mhando


Mkuu wa Wilaya Korogwe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa akitoa taarifa ya hali ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Korogwe
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama
Baadhi Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Korogwe





Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akitoa Maelekezo kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Mrakibu Mwandamizi Mbaraka Batenga Kuhusu Umuhimu wa Vizuizi


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Korogwe

Baadhi ya Askari wa Uhamiaji Wilaya ya Korogwe wakimsikiliza kwa Makaini Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala 



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Korogwe (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni