Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

17 Novemba 2020

UHAMIAJI Mtwara Yatoa Mafunzo ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba

Mtwara, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara imetoa Mafunzo ya kiuhamiaji kwa kuruti wa Jeshi la Akiba (Mgambo), Mkoani humo, Jumla ya kuruti 107 wa Jeshi hilo walipatiwa mafunzo hayo ambayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba katika kata ya Raha leo  Wilaya ya Mtwara Mjini huku wakiwa wiki ya  10 ya mafunzo yao ya miezi 03.

Elimu hiyo ilitolewa na Ofisa Kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kitengo cha Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Mwangolombe ambae alifundisha maana ya Uraia, Mhamiaji ni nani na Madhara ya kuwaficha wahamiaji haramu sanjari na kuwafundishwa mbinu za kuwbaini Wahamiaji haramu ikiwemo na kuwakumbusha umuhimu wa wao kushiriki katika  suala zima la ulinzi na usalama wa Taifa.

Katika kuendelea na juhudi hizo za kupambana na changamoto ya Wahamiaji Haramu hapa nchini Idara ya Uhamiaji inaendelea pia kutoa elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa Wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mitandao ya kijamii, machapisho, mikutano, na warsha mbalimbali ili kujenga uelewa wa Wananchi juu ya athari za kuwakumbatia wahamiaji haramu.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Mwangolombe Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Mtwara
Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Mtwara wakimsikiliza kwa Makini Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Mwangolombe Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni