Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

16 Novemba 2020

UHAMIAJI Iringa yatoa Elimu ya Uhamiaji kwa Jeshi la Akiba

Iringa – Tanzania


Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa chini ya Afisa Uhamiaji Mkoa Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACI Agnes Michael Luziga imeendelea kutoa elimu ya Kiuhamiaji katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa huo.

Lengo kuu la elimu hiyo ni kupambana na wimbi la wahamiaji haramu na kuwezesha kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo  ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya Kiuchumi.

Utoaji wa Elimu hiyo ya Uhamiaji umefanyika katika Mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) yanayoendelea katika Viwanja vya Mlandege vilivyopo Iringa Mjini, ambapo zaidi ya Kuruti 79 wa Jeshi hilo wamepatiwa elimu ya kiuhamiaji, ikiwemo Uraia, Pasipoti, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka ya Nchi.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Maafisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa yakiongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji A/ISP Omaru Mohamed na Afisa Uhusiano Uhamiaji (M) Konstebo Mariam Simba.

Aidha Jukumu la Ulinzi na Usalama wa Taifa letu ni la Kila Mtanzania, Katika zoezi la kupambana na wahamiaji haramu, Wananchi wanaaswa kushiriki  kwa kutoa taarifa katika Ofisi za Uhamiaji pindi wanapokutana na mtu au kundi la watu ambao wanawatilia shaka  katika maeneo yao ya kazi  ama makazi yao ili kuwezesha idara kuchunguza na kubaini sababu za ujio wa shughuli zao hapa nchini.

 HABARI PICHA NA MATUKIO

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Omaru Mohamed  (Kushoto) Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa kushoto kwake ni Mkufunzi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Omaru Mohamed Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa


Afisa Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa Konstebo Mariam Simba akifundisha Moja ya Mada za Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa (Hawapo Pichani)

Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa wakipata elimu ya Kiuhamiaji(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni