Dodoma, Tanzania
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala mapema leo hii amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya Ujenzi inayofanywa na Jeshi la Magereza Nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa Miradi ya serikali inayoendeshwa kwa njia ya “Force Account”
Ziara hiyo Imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza nchini na kutembelea Miradi katika Gereza la Isanga na Msalato Jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala katika ziara yake aliongozana na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Utawala na Fedha (CI) Edward Chogero, Mfawidhi wa Kitengo cha Majengo Mrakibu Justice Kusiluka na Mkuu wa kitengo cha Manunuzi na Ugavi Bwana Abdul Ndege.
CGI Dkt. Anna Makakala Amelipongeza Jeshi la Magereza Nchini kwa ubunifu na uthubutu wa kubuni miradi mbalimbali ambayo imetekelezeka kwa muda mfupi na kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Suleiman Mzee alisema kwa sasa Jeshi la Magereza limekuja na Mpango mkakati wa kuhakikisha Jeshi hilo linajitegemea kwa chakula na pia kwa kuendesha miradi mbalimbali ambayo inatekelezeka kwa faida ya Jeshi hilo na Taifa kwa Ujumla.
Akizungumza kwa nyakati Tofauti CGP Mzee alisema Jeshi la Magereza kwa sasa ndani ya Jiji la Dodoma limetekeleza mradi wa Nyumba 20 za kuishi Maafisa na Askari, Ujenzi wa Kiwanda cha Samani kilichopo katika Gereza la Msalato, Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo katika Eneo la Msalato, na Mradi wa Utengenezaji wa Matofali ambayo huuzwa kwa wateja mbalimbali na mengine kutumika katika ujenzi wa miradi ya Magereza.
Ziara ya CGI Dkt. Anna Makakala imekuwa yenye Mafanikio Makubwa ikiwemo Kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana uzoefu katika kazi sanjari na kudumisha uhusiano mwema uliopo baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala aisain i Kitabu cha Wageni katika eneo la Ujenzi wa Mradi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi La Magereza |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala Kushoto akiongozana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini CGP Suleiman Mzee katika Ukaguzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi La Magereza |
![]() |
Ziara Ikiendelea |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akifurahishwa na Mandhari ya baadhi ya Maeneo ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Nchini |
![]() |
Baadhi ya Nyumba za Jeshi la Magereza zilizokamilika Tayari kwa Matumizi ya Maafisa na Askari ambazo zimejengwa hivi Karibuni katika eneo la Gereza la Isanga Dodoma |

![]() |
Muonekeno wa Nyumba Mpya za Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Isanga Jijini Dodoma |
![]() |
Mradi wa Matofali wa Jeshi la Magereza |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Suleiman Mzee akimuonesha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala (Hayupo Pichani) baadhi ya Bidhaa zinazotengenezwa na Magereza |
![]() |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni