Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

20 Novemba 2020

DCI Towo Ahitimisha Mafunzo ya Usimamizi wa Masuala ya Ki-Uhamiaji Kwa Taasisi za Umma na Sekta Binafsi.

Moshi, Kilimanjaro

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdallah Towo mapema leo hii amehitimisha  mafunzo ya siku 05 ya usimamizi wa masuala ya Ki-Uhamiaji kwa taasisi za Umma  na sekta binafsi hapa nchini. 

Mafunzo hayo yamefanyika Katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro huku yakihusisha Washiriki wa Kundi la Tisa  (Oparesheni Matokeo).

DCI Towo alieleza kwamba mada zilizofundishwa na kujadiliwa zililenga katika kutafuta njia muafaka ya kuboresha huduma za Ki-uhamiaji.

“Ni wazi kwamba sisi sote tuna wajibu wa kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuweza kufanikisha sera ya taifa ya Tanzania ya Viwanda katika zama hizi za Uchumi wa kati kama inavyosisitizwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli” Alisema DCI Towo

Aidha amempongeza na Kumshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Peter Makakala kwa kuhakikisha kwamba mafunzo haya yanafanyika kama yalivyopangwa na pia kuhakikisha kuwa mafunzo wanayoyapata washiriki yanaleta tija kwa serikali na sekta binafsi kwa ujumla.

Katika Mafunzo hayo ya siku 05 Washiriki walipata fursa ya Kufanya ziara ya Kimafunzo katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), na kupata muda mzuri wa kujifunza mambo kadha wa kadha yahusuyo Mlima huo na mazingira yake.

Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kitaendelea kutoa  ushirikiano wa karibu kwa wadau wote wa sekta binafsi na tasisi za Umma ili kuweza kufanikisha malengo yake na kuhakikisha kuwa wadau wote wanafanya jambo moja lenye kuleta ufanisi na maslahi mapana kwa Ulinzi na Maendeleo ya Taifa letu.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo (Katikati) akiwa katika Picha ya Pomoja Wahitimu wa Mafunzo ya Usimamii wa Masuala ya Ki-Uhamiaji kwa Taasisi na Sekta Binafsi

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo akiwa Katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mafunzo ya Ki-Uhamiaji 



Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo akimkabidhi cheti mmoja wa Washiriki wa Mafunzo



Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo (hayupo Pichani)






Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Kutoka Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA (Kushoto) Mrakibu Msaidizi Leslie Mbotta akitoa maelekezo kwa Timu yake ya Itifaki katika eneo la Hifdhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)


Maafisa, Askari na Wahitimu wa Mafunzo ya Kiuhamiaji wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Lango kuu  la Marangu ambalo hutumika  Kuingilia Katika Kupanda Mlima Kilimanjaro



Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Kutoka Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA (Kushoto) Mrakibu Msaidizi Leslie Mbotta akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa Wahitimu wa Mafunzo yya Kiuhamiaji waliowasili katika Hifadhi ya KINAPA  Kwa lengo la Kujifunza



Baadhi ya Wahitimu wakiwa katika  Mfano wa Mlima Kilimanjaro




Afisa Utalii Daraja la Kwanza  Herman Mtei kutoka Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro  akitoa Maelezo na Historia ya Mlima Kilimanjaro wahitimu wa Mafunzo ya Masuala ya Kiuhamiaji (Hawapo Pichani)













(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Maoni 1 :